WAZEE CCM WAKERWA NA KAULI YA NAPE KWAMBA “WANASUBIRI KUFA”


Nape amejikuta katika mgogoro mzito na wazee ndani ya chama hicho baada ya gazeti moja kumnukuu akitamka kwamba wanaoshabikia mfumo wa serikali tatu katika kujadili rasimu ya Katiba mpya, ni “wazee wanaosubiri kufa”.

Baadhi ya wazee na makada waandamizi wamekerwa na kauli ya Nape, wakisema inaonyesha jeuri isiyo ya kawaida kwa kijana mdogo kama yeye.

Miongoni mwa wanaodai kukerwa na kauli hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji, Joseph Warioba, na waasisi kadhaa wa CCM wakiwamo Joseph Butiku, Jaji Mark Boman, Dk. Salim Ahmed Salim, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na wengine, hata wale wasiounga mkono hoja ya serikali tatu.

Hata hivyo, Nape anadaiwa kuwa amepiga simu kwa baadhi ya wazee hao kuwaomba radhi na kukanusha kauli hiyo, akidai kuwa alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari.

Baadhi yao wanasema hata kauli ya majuzi ya waziri mstaafu, Mateo Qaresi, ya kuiponda serikali na uongozi wa CCM, imetokana na hasira dhidi ya kauli ya Nape, ingawa msimamo wake juu ya mfumo wa muungano wa serikali ni ya siku nyingi.

Waziri huyo mstaafu amenukuliwa akisema, “Hivi hawa viongozi wanajua tunakoelekea, leo hii ukiulizwa dira yetu ni nini hakuna anayejua, bali tunajiendea tu,” kauli ambayo imeibua hisia kali ndani ya serikali na CCM.

Source:Tanzania Daima
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MPIGENI JUJU AANZE KUFA YEYE ,KALEWA MADARAKA DOGO HUYO


    ReplyDelete
  2. Magezeti ya tz nayo yame ktgamtgmgtj

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad