Katika mechi ya Yanga iliyopigwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, Vijana wa Jangwani walitawala mchezo tangu mwanzo mpaka
mwisho, huku Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora Rangers wakilazimika
kukomboa mabao baada ya kutangulia kufungwa mara mbili.
Iliwachukua Yanga dakika 10 tu tangu kuanza mchezo
kufunga bao la kwanza lililowekwa kimiani na Jerryson Tegete
aliyemalizia kwenye kamba pasi nzuri ya Simon Msuva na kumtungua kipa wa
Ashanti, Ibrahim Abdallah.
Hussen Sued kuzuiwa na Tegete kabla ya kuvuka mstari huku tayari Kipa Ally Mustapha akiwa ameshapitwa na mpira.
Ashanti walikuwa na nafasi nyingine ya kusawazisha
dakika ya 24 kufuatia shuti kali la Sued kumlazimisha Mustapha kufanya
kazi ya ziada kulipangua na kuwa kona.
Dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili,
Msuva aliipeleka Yanga mbele na kufanya matokeo kuwa 2-0, kabla ya
Tegete kufunga bao la tatu dakika ya 57, na kisha Haruna Niyonzima
kufanya matokeo kuwa 4-0 dakika ya 73.
Ashanti walifunga bao la kufutia machozi dakika ya 90 kupitia kwa Shaaban Juma, kabla ya Nizar Khalfan kufunga nao la tano.
Akijitetea na kipigo hicho, Kocha wa Ashanti Hassan Banyai alisema kikosi chake kinahitaji muda zaidi.
Tabora:
Mjini Tabora, Simba wakishangiliwa na umati
mkubwa, walibanwa vilivyo na wageni wa Ligi Kuu, Rhino Rangers na
kulazimisha sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Katika mechi hiyo iliyochelewa kuanza kufuatia
utata wa vibali vya wachezaji, Joseph Owino, Abel Dhaira na kukosekana
kwa leseni ya Betram Mwombeki, timu zote zilishambuliana kwa zamu.
Iliwachukua Msimbazi dakika 8 tangu kupulizwa
filimbi ya kuanza mchezo kufunga la kwanza kupitia Jonas Mkude
aliyeunganisha kwenye kamba kwa
kichwa kona maridadi ya Issa ‘Baba Ubaya’ Rashid.
Wenyeji Rangers walisawazisha bao hilo dakika ya 35 kupitia Iman Noel
aliyepiga mpira wa adhabu ndogo na kwenda moja kwa
moja wavuni, kabla ya dakika moja baadaye Simba kuongeza bao la pili
likifungwa na Mkude kwa kiki ya penalti.
Penalti hiyo ilitokana na kiungo Amri Kiemba
kuchezewa faulo ndani ya eneo la hatari na beki wa Rangers, Daniel
Manyenya, aliyeishia pia kuonyesha kadi ya njano kwa kosa hilo.
Sekunde chache kabla ya mapumziko, Rangers
walifunga bao la kusawazisha, ambalo lilikataliwa na Mwamuzi Amos Paul
kutoka Mara kwa madai kuwa kabla ya bao hilo, kipa wa Simba alifanyiwa
madhambi.
Kipa wa Rangers, Abdul Mtumwa alifanya kazi kubwa
kuokoa mpira wa kichwa kutoka kwa Joseph Owino kufuatia kona
iliyochongwa na Baba Ubaya dakika ya 20.
Kipindi cha pili, Rangers walibadilika na kufanya
mashambulizi makali na kufunga bao la kusawazisha dakika ya 70 kupitia
Stanslaus Mwaktos aliyefunga kwa kiki ya adhabu ndogo iliyomponyoka kipa
wa Simba.