AGNESS MASOGANGE NA MDOGO WAKE WAACHIWA HURU KABISA..TUTAKOMAJE MTAANI

Tegemea picha zaidi za ‘asset’ ya Agnes Gerald aka Masogange kwenye Instagram sababu video vixen huyo ni mtu huru kabisa.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo, Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini imemwachia huru mrembo huyo baada ya kulipa faini ya R30,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 4.8 za Tanzania, kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.

Naye Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wowote wa kumtia hatiani.

Habari hiyo kwenye gazeti la Mwananchi inaeleza kwa urefu:

Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Mahakama hiyo ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.

“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” gazeti la Mwananchi limemnukuu Kapteni Ramaloko.

Alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.

Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).

Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.

Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.

Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya

Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.

Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.

Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.

“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu,” alisema Muller kwa kujiamini.

Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.

“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema Nzowa.

Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.

“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema Nzowa.

Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.

“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini,” alisema.

Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi.

Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.

Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.

Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani.

Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege.

Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.

Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.

Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini.

Source: Mwananchi

Post a Comment

27 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mtajuwana wenyewe hasa wale maofisa walokwenda s.africa ndio walokwenda kuucheza huu mchezo.

    ReplyDelete
  2. Dah! Yaan watz 2mefanywa wajinga kias hk!!! Hii kweli serikal ya viongoz wauza unga....bora uhalalishwe 2jue moja 2 coz serikal yenyewe ndo mna2uuzia sembe.

    ReplyDelete
  3. Yaan ni ushenz unaotia hacra jaman ila bac tu maisha yanasonga

    ReplyDelete
  4. Mwakyembe kwa stail hii 2naomba uwarejeshe kazn haraka xana wale wote uliowafuza kaz pale airpot mana walipitisha mzgo halal. Huu c usenge kumamae zenu viongoz we2 mliofuatilia hii issue mana mnatuletetea usenge wa waziwaz. Wote wauza unga nyinýi kama we nzoa mungu akulaani hadi unaingia kabuln unaenda sauz unarud unatalutetea huu uxenge!!! Unatumiwaaaaaaa.... Msonyoo

    ReplyDelete
  5. Yeaah........welcome back baby i missed u sana jamani i cant wait to see wewe,mmwaaaa!!

    ReplyDelete
  6. Kweli kamanda nzoa ni msenge sana alaniwe milele

    ReplyDelete
  7. Unalolote teja wewe.subir anakuja kukuzia kete mana ulimiss kunesa.

    ReplyDelete
  8. Alafu eti nzoa anjaidai kushangaa eti adhabu walopewa ni ndogo mnafk mkubwa ww.

    ReplyDelete
  9. Mamae walah inauma jmn duuh,huu ni ufraun uliopitiliza,yaan nmechokaje mwili mzima,duuh ukundu wa hali juu sana

    ReplyDelete
  10. Hii ni dhahiri madawa ya kulevya inavyooshesha yaruhuaiwe tu ni umburula kiasi gani leo tunaambiwa amekamatwa na madaya ya kulevya kesho mnaambiwa yalikuwa makemikali na sio dawa kweli serkali hazina macho hazioni na kiziwi hazisikii kabisa nasema adhaa kanoon sheria kipofu haioni

    ReplyDelete
  11. Daaahh kumanina zao,hawajamaa wote wasenge watupu,yaan mtu anakamatwa na madawa halafu wwanamuacha kisenge hivyo,khaaa..bora iwe biashara huru tu tujue moja.Wote mikundu!!!!

    ReplyDelete
  12. Waachiwe tu tutawaadhibu hukuhuku kitaa wasing'ae mtaani wasenge hawa tutawakomesha,ndugu zetu walivoharibika kwa hiyo midawa yenu.mtakiona.na 2015 kitaeleweka tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sure mdau hasira zooooooote 2015 kitaeleweka maanina zao...

      Delete
  13. duh africa bara moto

    ReplyDelete
  14. Ok hadi tuchukue sheria mkononi eee subiri kiitaa wauza unga woooote tutawapiga mawe km wezi nyie endeleeni kuwapa kichwa....

    ReplyDelete
  15. Nzoa ujihuzuru haraka sana,haiwezekani iwe kichwa cha mwendawazim kias ki hik

    ReplyDelete
  16. Hakuna ambae hajakasirishwa na hili swala hasa wakati huu wa mapambano dhidi ya hizi dawa,hata awe mtoto hawez amin kilichofanyika.hili taifa la unga tuendelee kuliombea libaki hivi hivi coz tumechoshwa na uongo wenu Wasenge tu viongoz wa taifa hili.anaetaka kunitumia kama punda plz nitafute kumbe mambo rahisi ivi!yaan rasm nataka kuwa punda.

    ReplyDelete
  17. Waingizien hadi mikunduni wazisafirishe afu habari zenu tafuten majarida maalum mziweke hatutaki kuzisikia kwny magazet yny habari mchanganyiko na blogers msituandikie hizi habari za kisenge ili tupende blog zenu vingnvy hazina maana

    ReplyDelete
  18. we nzowa mungu anakuona, we ndo umeenda kucheza mchongo wote, mbona wafungwa wengine wa dawa za kulevya haukwenda kuwahoji, shame on you nzowa.

    ReplyDelete
  19. Hawa wanatakiwa kushitakiwa Tanzania kwa kuexport controlled substance without permit and permit.

    ReplyDelete
  20. Dada zetu wakifika Tz wanyamaze kusema maneno yakulumbana, vijembe hayatawasaidia huu ndio ushauri wangu

    ReplyDelete
  21. wadau kama hapa bongo wataachiwa hawa watu hyo nzowa na mwakyembe wajiuzulu wao na washtakiwe wao

    ReplyDelete
  22. Hiii ndo tz full uharamu na u fek fek.kama nchi imerogwa vile?nyerere uko uliko hii ndo tz ulioiacha.kila mtu anaishi atakavyo,taifa la wauza unga dah inaumiza sanaaaaaaaaaaaa.na yana mwisho wake haya.

    ReplyDelete
  23. bushoke aliimba kweli...jiulize kwa nn walio jela wengi maskini? Papii kocha na Nguza vick wanazeekea jela wakati mipunda tena imekamatwa live eti inaachiwa..dah ila malipo hapa hapa duniani

    ReplyDelete
  24. Dah! Mdau hapa umenitoa choz.. wallahi

    ReplyDelete
  25. kweli nowma watu wote hapa comment zao zinamanisha mwenzao afungwe yani alivyo achiwa atu wanaona hatari kweli

    ReplyDelete
  26. bora arudie ile kazi yake ya kujiuza buguruni kuliko poda

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad