AIBU..!. MUME AMRUHUSU MKEWE AJIUZE ILI WAPATE PESA YA CHAKULA...!

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, hivi karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina.
Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.

Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu baada ya wanahabari  kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.

Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa , ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:

“Pigeni hizo picha mnadhani nani ana wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula.


“Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu akiona picha zangu ataniacha mmenoa. Mume wangu yeye anajua niko wapi saa hizi, hata nikichelewa kuja huku usiku yeye ndiye hunihimiza ili nije kupata pesa.”


Mwanamke huyo aliyatoa maelezo hayo kwa ujasiri mkubwa na bila kujali kwamba anapigwa picha huku akiwa ameshikilia upande wa khanga.

Baadhi ya majirani waliposikia mkwara wa mwanamke huyo walitoka kushuhudia lakini walipokutana na mwanga mkali wa kamera   walirudi majumbani mwao na kujifungia milango huku wakidai hayawahusu .

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umaskini ulaaniwe!



    Bijou

    ReplyDelete

  2. Jamani huyo jamaa kama ni kweli alimruhusu basi kapinda balaa

    ReplyDelete
  3. Mwongi huyo mwanamke

    ReplyDelete
  4. Inawezekana kabisa, maana kuna jamaa mtaani kwetu yeye ni kibaka mzoefu na mkewe anajiuza. Kila mmoja anafahamu kaz ya mwenziwe na wako poa sn. Dunia kushneeiii...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad