AIBU:MUME ANASA PICHA ZA MKEWE AKISALITI NDOA NA MWANAUME MWINGINE GESTI

Haruni Sanchawa na Gladness Mallya
NI aibu! Mwanaume mfanyabiashara wa jijini Dar aitwaye Joseph Mboje, amenasa picha za mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Rehema akimtuhumu kusaliti ndoa yao na mwanaume mwingine.
Rehema Mboje akiwa na mwanaume mwingine.
Mboje alidai kuwa kwa muda mrefu alikuwa akimhisi mkewe ‘kucheza nje kapu’ na mwanaume mwingine ambapo katika pekuapekua yake ndipo akanasa picha hizo kwenye simu yake kabla ya hivi karibuni kutengana kabisa.
Kwa mujibu wa Mboje, baada ya kumgundua na kunasa matukio yake na mwanaume nje ya ndoa hasa gesti, mkewe huyo aliondoka nyumbani maeneo ya Manzese, Mtaa wa Sisi-Kwasisi, Dar, bila kujua alikohamia lakini alipofanya uchunguzi akabaini ana mwanaume mwingine.
Mke wa mtu, Rehema Mboje akiwa amelala gesti.
“Sikuacha kupeleleza, nikaambiwa na mtu wangu wa karibu kuwa chanzo cha mke wangu kuondoka nyumbani ni kijana mmoja tuliyewahi kumwajiri katika biashara zetu,” alisema Mboje.
Huku akizungumza kwa uchungu, jamaa huyo alisema kuwa kijana huyo aliletwa na mkewe kama meneja wa baa yao iliyopo Kinondoni-Mkwajuni, Dar lakini baada ya muda aliona mabadiliko makubwa kutoka kwa mkewe, jambo lililomshtua kwani alianza kuwa mlevi wa kupindukia na kurudi nyumbani usiku wa manane.
Mume wa Rehema, Joseph Mboje.
Alidai kuwa baada ya kushtuka, alimuuliza mkewe huyo kuhusiana na hali hiyo ya kuvuka kiwango hadi kujifotoa akiwa na mwanaume nje ya ndoa lakini alikana.
Mboje alidai kuwa aliendelea kufuatilia nyendo zao kwa kipindi cha miaka mitano, mwaka wa sita ambao ndiyo huu, mambo yakawa wazi kuwa mkewe wa ndoa aliyedumu naye kwa miaka 17, anatembea na kijana huyo aliyemtaja kwa jina moja la Lwalwai.
“Nimeumia sana, sikutarajia kama mke wangu anaweza kunifanyia hivi,” alisema.
Rehema akiwa gesti.
Rehema alipotafutwa na gazeti hili, alianza kwa kumkandia mumewe na kusema hamtaki tena.
Alipobanwa na wanahabari wetu, alikiri kuwa Mboje alikuwa mumewe na kwamba amezaa naye watoto wawili na kuishi pamoja kwa miaka 17 kabla ya ndoa kuvunjika.
Alisema kwa sasa maisha aliyoamua kuishi anayajua mwenyewe hivyo kila mtu achukue hamsini zake.
Mwanamke huyo pia alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Lwalwai tangu kipindi cha nyuma na hii yote alifanya kutokana na tabia za mumewe ambazo hakutaka kuziweka wazi.
Alisema kwa sasa anaishi peke yake na kama huyo mumewe ataanza kumfuatafuata huenda akaamua kuolewa na Lwalwai.
Kwa upande wake, Lwalwai alisema kuwa ni kweli alikuwa na uhusiano na Rehema lakini hakujua kama ni mke wa mtu ndiyo maana alikubali kushirikiana naye kimapenzi pamoja na kuwa alikuwa anafanya kazi kwake.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dunia imesha ishaga zamani..nahisi ndo ina malizikia..Mrejee Mungu wako kabla hayajakukuta

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad