AISHA BUI: SIJAFUNGWA KWA ‘UNGA’ BRAZIL..NIPO NAENJOY NA MCHUMBA HUKU

HUKU kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na kufafanua juu ya tuhuma hizo.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake hakuwa tayari kulianika.
“Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu.


“Wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya.
“Naomba Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hiv shigongo utaacha lin kuchafua wenzio? Shigongo mgeukie Muumba wako ww mbona Mzee Machache ns k linny +ruge zama na ray c unawaogopa?

    ReplyDelete
  2. pole asee kwa kuchafuliwa...c unajua wa2 wanataka wauze magazet... na blog nazo wana2mia habari kama hiz kutangaza blog zao nao waonekane wako update na newz

    ReplyDelete
  3. Sintah aibu yako si ulisema amefumgwa kipo wapi sasa

    ReplyDelete
  4. Amna lolote wote ndo walf wale 2 kasoro majina

    ReplyDelete
  5. hivi we fala hapo juu kwani umesikia sintah ndo kacreate hiyo habari? yeye alipost kwenye blog yake siku 1 baada ya mablog kibao kupost hiyo story..acha chuki binasfi, povu linakutoka kama umekunywa juice ya omo..mxuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad