AMNYWESHA MWENZAKE VIROBA KISHA AMLAWITI

JESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.

Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.

“Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha na kupoteza fahamu,” alisema.

Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.

Alisema kuwa wasamaria wema walimshuhudia mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama huo dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu kumkamata, aliwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.

“Raia wema hao walimbeba muathirika na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye aliweza kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu makali sehemu yake ya haja kubwa,” alisema.

Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. POMBE SI CHAI JAMANI.
    MWANAUME MZIMA WAENDA KUNYWESHWA POMBE.
    HIYO NDO FAIDA YA KUPENDA VYA BURE. BAAYHI YA WANAUME WA SIKU HIZI WANA ROHO YA SHETANI, NDO WANAOBAKA WATOTI NA KUWALAWITI. NI DHAMBI NA AIBU KUBWA KWA WOTE WAWILI.

    ReplyDelete
  2. Mh!jamaniiii yani kam cameroon mwenzie....!nawe ulibweteka mno,cheki sn ucjekuta unamuonekano wa kishoga.

    ReplyDelete
  3. aiseeeeeeee wapenda vya bure mmeiyona hiyooo,,,,kula bure,,liwa tigo bure..sani safiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  4. wa2 wanaogonga tgo na wanaogawa tgo kwa hiari yao wanamatatzo ya akili

    ReplyDelete
  5. nahisi waliafikiana hao,wasituzuge hiyo kitu hadi uje uumizwe kiasi hicho hujagutuka tu,halafu mjeruhiwa huyo mbona kama mzoefu vile.

    ReplyDelete
  6. Acheni uongo picha na maelezo yenu ni vitu viwili tofauti kabisa.

    ReplyDelete
  7. mbona wa kwenye hiyo picha nawajua ni mashoga maarufu mjini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad