BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa.
Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam.
Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani.
‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.
Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao.
Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili yao, wataacha kujiuza.
BAADHI YA MAWAZIRI NA MAPOLISI WATAJWA KUWA NDIO WATEJA WA MACHANGUDOA
2
September 06, 2013
Tags
Ni kweli eti kama wanaume wakiacha kuwanunua wataacha hiyo busnez. Jiepusheni jamani tuache tamaa ya muda mfupi. Ukatesa familia na jamaa zako kwa kuendekeza ngono. Mbona Africa tuko hivi jamani....
ReplyDeleteshida si o afrika ni dunia nzima,heri hata afrika kuna nafuu ,wanaume wananyanyaswa sana ,wengine hawapewi tunda hatakama wameoa,km huna Mungu unategemea nini? huku wana ume ndio wanakimbia wanawake,wengi wana magari na kazi nzuri ,ni tabia tu? wana watoto,na biashara,pia ni sehemu ya interest za watu wengine,wengine wanatafuta weusi,wengine,waspanishi,ilimradi kila mtu anatafuta shetani yuko wapi? ni maombi ,na watu kubadilika wala sio swali la kipato ulaya au amerika ni tabia na utalii wa ajabu unaoendelea sasa,huwezi kuamini hali ilivyo huku magharibi ni mbaya sana,tv,inter net nazo zinachangia,na elimu ya mahusiano pia,Mungu atusaidie Tanzania tumrudie Mungu ndio njia salama.
ReplyDelete