BALAA:HAKIMU ACHOMWA KISU MAHAKAMANI

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.

Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.

Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.

Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.

Hata hivyo, baada ya kutoa maelezo, si mshtakiwa wala mdhamini wake aliyehudhuria mahakamani hapo licha ya kesi hiyo kusikilizwa mara mbili bila ya taarifa yoyote kabla ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo jana.

Kushambuliwa

Baada ya hukumu hiyo mlalamikaji alitoa shukrani na kuwashika mikono wote waliokuwamo mahakamani humo na kutoka nje.

Ilidaiwa kuwa baada ya dakika 15, Izengo alirudi mahakamani hapo na kudai kuwa ameleta risiti ya kumwonyesha hakimu thamani ya baiskeli yake alipoingia ndani ndipo kelele za Mshauri wa Baraza, Mary Wamba zikaanza kusikika akisema: ‘Njooni jamani hakimu kavamiwa anapigwa’.

Baada ya watu waliokuwa karibu kuingia katika ofisi ya Mahakama hiyo walikuta hakimu ameshacwhomwa kisu katika shavu la upande wa kushoto huku akivuja damu nyingi huku mtuhumiwa huyo akiendelea kumshambulia. Baada ya tukio hilo, wasamaria wema walimpeleka hakimu huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema mtuhumiwa alikamatwa mara baada ya tukio hilo kusubiri hatua za kisheria dhidi yake.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamaa
    anaonekana alinunua baiskeli yake kwa kutoa jasho sana,sasa anaona
    wanataka kuipoteza kirahisi rahisi!sio vizuri kabisa kuna haja ya
    mahakama kuwa zinatenda haki ili kuepusha vitu kama hivi!

    ReplyDelete
  2. polisi ni wazembe sana,mtu anaingia na silaha mahakamani mpaka hakimu anajeruhiwa?bila shaka huwa hawakaguliwi

    ReplyDelete
  3. kwakawaida mahakama zamwanzoahakimu huwa hatendi haki huyu jamaa alijua anataka kuchezewa keusi ikabidi ajikimu.m.ng.machimkenda

    ReplyDelete
  4. Ivi hii sheria ipo ya kumhukum mtu ambae hajulikani alipo?wanasheria mtusaidie hili

    ReplyDelete
  5. Mahakimu mmezidi kupindisha haki za watu. Hiyo ni intro na bado yatawakuta makubwa zaidi ya hayo watu wamewachoka.

    ReplyDelete
  6. Mahakama za hapa ,ma,huwezi kwenda mahakamani ,na silaha ,unakaguliwa,hata ufunguo ,na kalamu ,mpaka ndani ya soksi ,dunia imebadilika ni lazima vyombo vya ulinzi vifanya kazi hata hospitalini,na mahotelini serikali si inawalipa ,hapa ktk vyuo vikuu,na mashule ni hali ya wanafunzi na walimu kulindwa,ndivyo wenzenu wanafanya hivyo huko magharibi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad