BATULI:NAMUOGOPA MAMA KANUMBA ..NIKIMUONA HATA KUMSALIMIA SIWEZI

Stori: Brighton Masalu
Staa anayesongesha maisha yake Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema akimuona mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa anaogopa hata kumsalimia kwa madai hukumbuka mambo mengi ya marehemu.
Akimwaga mawili matatu mbele ya kinasa sauti chetu,  maeneo ya Kinondoni, jijini Dar, Batuli ambaye aliibuliwa na marehemu Kanumba kwenye filamu ya Fake Smile, alisema kamwe hawezi kuondoa uwepo wa marehemu katika ubongo wake na ndiyo maana anaogopa hata kumsalimia mama Kanumba.
 “Ukweli ni kwamba bado sijawa na ujasiri wa kumkabili mama huyo, huwa nakumbuka mambo mengi sana kila nikimuona, naishia kumkimbia tu, hata pale Kariakoo juzikati niliogopa kabisa kumsalimia kwani ningeishia kulia mbele ya umati,” alisema Batuli.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huna lolote unamuogopea nini sasa unalako jambo

    ReplyDelete
  2. Mbona mambo ya kawaida ww unaogopa nn! acha utoto ww inatakiwa uzoee japo hayazoeleki.

    ReplyDelete
  3. mbona kuna vitu vingi vya kuandika jamani tena vya maendeleo, kwa nn kila siku ujinga huu, so what kama anamuogopa? kila gazeti batuli batuli, tumechokaaaaaaaaa!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad