BEEF LA UWOYA NA SHIGONGO..GLOBAL PUBLISHERS WAMCHANA TENA UWOYA..SOMA HAPA

Na Luqman Maloto

BINAFSI nafahamu kwamba Irene Uwoya aliwahi kuwa staa mkubwa nchini lakini akafanya makosa na sasa ameshuka chati. Ameporomoka kwa kiasi kikubwa sana.



Elizabeth Michael ‘Lulu’, baada ya ‘ajali’ yake na marehemu Steven Kanumba, alikaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini baada ya kutoka ameonekana kuwa na mafanikio makubwa kuliko Uwoya ambaye siku zote yupo mtaani.
Pengine kuna aina fulani ya maisha ambayo Uwoya amejichagulia maana akina Rose Ndauka, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu na wengineo wamekuwa wakifanya vizuri, wanamfunika sana. Ameshindwa kujisahihisha, ataendelea kusugua.
Najua kwamba Uwoya ana hali mbaya kisanii, amechoka, muonekano wake hausisimui tena, amepoteza mashabiki, kwa maana hiyo hauzi. Dili za kucheza filamu zinaota mbawa kila kukicha, maprodyuza wanataka wakali ambao wanafanya biashara sokoni.
Naelewa kuwa hivi sasa katika ulimwengu wa masupastaa, Uwoya amebaki msindikizaji lakini sikuwahi kufikiri kwamba anaweza kufikia hatua mbaya kiasi hicho. Kafikishwa mbaroni kwa wizi wa simu? Yaani wizi wa simu ya mkononi! Anatia huruma.
Yamemfika yapi? Sitaki kuamini kama Uwoya anashindwa kununua simu halali. Akili nyingine inaniambia kuwa hawa dada zetu wanaharibiwa na uchu wa kupenda vitu vya juu lakini uwezo ni mdogo. Je, huo wizi wenyewe alifanyaje?
Atakapofikishwa mahakamani pengine itajulikana kama kweli amehusika na wizi huo, basi itafahamika ameufanyaje. Ni yeye moja kwa moja au kupitia kwa mtu mwingine? Dunia ina mengi, ni vizuri hili jambo likafika kortini, huko tutajua ukweli halisi.
Swali langu ni hili, kama kweli ile simu alinunua kwa nini pale kituoni hakutoa risiti? Hata kama ingekuwa nyumbani, alishindwa nini kuagiza aletewe kuthibitisha kama ni mali yake? Maswali hayo mawili yanaongeza uzani kwenye madai kwamba ile simu ni ya wizi.
Ni ya wizi sawa, je, ni kweli Uwoya anaweza kuiba simu? Inawezekana kabisa akatega Kariakoo halafu amvizie mtu na kumchomolea? Maana mashtaka dhidi yake ni Wizi wa Maungoni, yaani wizi wa kumchomolea mtu kitu kutoka mwilini.
Kesi ipo Msimbazi Polisi na imeandikwa kwenye kitabu cha ripoti za kumbukumbu (report book ‘RB’) kwa nambari MS/RB/8522/2013. Hata hivyo, simu yenyewe iliyoibwa ina thamani kubwa, nahisi Uwoya aliinunua kwa mtu ambaye ndiye mwizi.
Mikono ya Uwoya na vidole vyake vilivyo, haoneshi kama anaweza kuwa mkali wa kuchomolea watu. Hata kama kaishiwa na kupigika, siyo rahisi akafanya hivyo. Sura yake haioneshi ushujaa wa ‘kupiga ndole’ lakini ya Mungu mengi.
Labda kauziwa lakini yeye ndiye kakutwa na mali ya wizi (aliyekutwa na ngozi ndiye aliyeiba ng’ombe). Kama ipo hivyo, hilo nalo ni tatizo kubwa. Maana yake yeye naye ni mmoja wa watu wanaowafanya wezi waendelee kufanya uporaji. Anawafadhili kwa mlango wa nyuma.
Tusimamie hapa kwamba kama alinunua, basi Uwoya ni mfadhili wa wezi kwa sababu mtu anayenunua mali ya wizi, anawasaidia wezi kuendelea kuishi kwa uporaji. Kwa maana hiyo siyo mtu mzuri, hafai kwenye jamii.
Kwa mwenendo huo, naamini ndiyo maana ameporomoka, anakosa sifa ya kuitwa kioo cha jamii. Inawezekanaje awe mfano wa kuigwa ikiwa yeye ni kirusi katika hiyohiyo jamii? Mtu unajua kabisa hii mali ya wizi unainunua kwa bei chee halafu unaona raha.
Kununua mali ya wizi ni hujuma nzito, ni ukosefu wa huruma kwa sababu wakati wewe unauziwa mali hizo kwa bei nafuu sawa na bure, halafu unaitumia kwa nafasi huku ukijionesha, mwenzako anateseka mno.
Fikiria kama wewe umejibana, ukajitutumua kununua simu aina ya iPhone 5 kwa shilingi milioni 1.6. Umeitumia wiki mbili tu unaibiwa, halafu mtu mwingine anakuja kuuziwa kwa shilingi 400,000  au 300,000. Itakuuma kiasi gani?
Bila shaka utamchukia mwizi na yule aliyeuziwa, kwani angekuwa muungwana asingekubali kununua. Laiti angekuwa raia mwema, angesaidia huyo muuzaji akamatwe ili aliyeibiwa arudishiwe mali yake. Kutumia mali ya wizi ni dhuluma, ni wizi.
Uwoya alikamatwa na simu ya wizi aina ya iPhone 5, kwa hiyo kama aliuziwa, na kwa mujibu wa tafsiri ambayo nimeielezea hapo juu ni wazi kwamba yeye siyo raia mwema. Ukweli uzidi kusimama kwamba hafai kuitwa kioo cha jamii.
Je, ni tamaa ya kutaka vitu vizuri wakati pesa hana? Ajioneshe mjini kwamba anamiliki iPhone 5 kumbe ni ya wizi, ameipata kimagumashi. Namshauri Uwoya aache mtindo wa kuishi kimagumashi, kama hana akubali hali halisi. Si kulazimisha maisha ya gharama, matokeo yake ndiyo haya.

ANGEMTII MUMEWE YASINGEMFIKA HAYA
Nikiongoza jopo la waandishi kutoka Global Publishers Ltd, mwaka jana, tulifanikisha kumsuluhisha Uwoya na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kutokana na mgogoro wa nguvu ambao ulikuwa unaitikisa ndoa yao. 
Malalamiko ya Kataut yalijikita katika uaminifu, kwamba Uwoya alikuwa anaonesha alama nyingi kuwa si mwaminifu kwenye ndoa yao. Mume huyo, alisema kwamba amenunua vifaa na kuanzisha kampuni ili mkewe ajisimamie katika kazi zake za filamu lakini mke hataki.
“Analipwa pesa kidogo ambayo akifanya shopping tu zinakwisha, maprodyuza wanapata fedha nyingi, yeye anafanya kazi, anauza sura tu lakini pesa hakuna. Nataka atengeneze filamu zake ili apate pesa za kuonekana lakini haelewi wakati kila kitu nimeshanunua,” Kataut alilalamika.
Kataut alikuwa na nia ya dhati kabisa ya kumwokoa Uwoya na pengine kama angefuata mwongozo wa mumewe leo hii asingeporomoka kama alivyo. Pengine yanayomkuta leo ni malipo ya kile ambacho alimtendea mwanamme huyo.
Mke wa mtu kunaswa hotelini na kijana wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ni aibu sana! Kabla ya hapo zilishaibuka stori kwamba amegombana na supastaa Jacqueline Wolper kisa mwanaume. Alimtesa sana Kataut wa watu.
Akiwa yupo ndani ya ndoa, akaingia kwenye mgogoro na boyfriend wake wa zamani, Hamis Ramadhan Baba ‘H-Baba’, akadai eti katika wanaume wake wote waliopita, ambaye hawezi kurudiana naye ni H-Baba. Huyu ni mke wa mtu.
Tafsiri; kumbe pamoja na kuwa kwenye ndoa, anaweza kurudiana na wanaume wake wote waliotangulia isipokuwa tu H-Baba. Je, unamuonaje huyo? Ni mke wa mtu kweli? 
Mke wa H-Baba, Flora Mvungi naye akamvaa Uwoya, akamchamba, wakachambana. Mke wa mtu anagombana na mwanamke mwingine kisa mwanaume tofauti na mumewe. Ninaposema hafai kwenye jamii namaanisha kweli.
Matukio ambayo anakumbana nayo hususan hili la wizi wa simu, achukue kama changamoto na ajisahihishe pale alipojikwaa. Amwangukie mumewe pengine mambo yakamnyookea. Iwe kama ameiba yeye moja kwa moja au aliuziwa, ajisahihishe. 

Source:Global Publishers

Post a Comment

36 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. longman .. acha upambe bongo simu kuuziana kiswahili bila risiti ni jambo la kawaida...hata wewe hapo hiyo simu yako kama una risiti sijui! na hata kama ulinunua ukapewa risiti sidhani kama bado unayo,wabongo hatujui kutunza document muhimu so swala la uwoya kushindwa kuonyesha risiti ni jambo la kawaida kabisaaaa hata wewe unajua hapa bongo!,,kuhusu umalaya wake .kumtesa mume hayo ni mambo yake binafsi na maisha yake muacheni mtoto wa watu ..hata wewe una mke ,una watoto wa kike ...una dada zako ...achana na maisha ya watu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upo sawa kabisa,wabongo tumezidi kufwatiliana badala ya mtu kufanya ya maendeleo.

      Delete
    2. Kweli fata yako yakusaidie.

      Delete
  2. mtaendelea kumchafua sana tutampenda milele.ndo nazid kuongeza km xa mbali za kununua magazet ya shigongo

    ReplyDelete
  3. Shigongo acha kumuandama mtoto wa watu

    ReplyDelete
  4. shigongo acha roho mbaya nyooooooooooooooo kakunyima papuchi una mwandama lol wewe baba huna haya unadhani yako hatuyajui na kile kibinti cha shule mwanza ulikuwa nacho tutamwaga data ohoooo

    ReplyDelete
  5. Nlilikua siamin kua global mna hila na uwoya ila sasa nimeamin,na mwandishi aliendika hi habar kama ni mwanaume una umelaaniwa,na kama ni mwanamke,nina hakika mtaa unaoishi utakua umevunja ndoa nyingi sana za wa2 kwa umbea,maana hiki hiki kipaji sijawai kuona

    ReplyDelete
  6. mwizi ni wewe shigongo na marehemu baba yako na mama yako mzazi ...nakutafuta tindikali inakuhusu wewe subili na uso wako ..yaani lazima tindikali

    ReplyDelete
  7. uwoya ataendelea kuwa uwoya hata umchafue vp me nataendelea kumpenda coz kila mwanadam anakosea

    ReplyDelete
  8. Jamani hayo majanga maskin uwoya sanaa te à vais kahaaribuuuu

    ReplyDelete
  9. Global mmeishiwa habari haina maana kabisa ni ya kuunga unga mpaka basi nia ni kumchafua tu. Hamwezi kumuangusha mtu ki hivyo ilhali nyie c mungu.

    ReplyDelete
  10. Shigongo wewe ni mpumbavu,kweli tunajua huyo dada ni changu,lakini kwa nini utumie kalamu yako ya uandishi kwa manufaa binafsi...Mungu na akulaani kwa sababu tunajua ugomvi wenu binafsi ni kitu gani...pole sana

    ReplyDelete
  11. Nimezikumbuka makala zilizokua zikiandikwa Enzi zile kabla Marehemu Amina Chifupa hajafariki asee dahh ni km hizi tuu kumuandama mtuu c vizur kutumia chombo binafc kumchafua mwingine badilikeniiii

    ReplyDelete
  12. Uzuri tunakujua wewe ni mwanafasihi so endelea tu na maumburula yako,tunajua kwa sasa unauza kupitia hako kastori ka dada yetu kuhusu simu koma,nyambafu mkubwa wewe

    ReplyDelete
  13. Jamani ila kama yalioandikwa ni uongo huyo uwoya si ana haki ya kuwashtaki global publishers. Ukiona kimya manake ni kweli.

    ReplyDelete
  14. Wewe ushuzi kukaa kmya ni jibu la mjinga jaman namkubali irene uwoya nw days amebadilika not kama zaman ila huyu shigongo ni mavi tu anafanya mambo ya kitotoooo

    ReplyDelete
  15. Shigongo hana tofauti na hahaha..mwanaume ndani una bikini...acha mambo ya wanawake mwenyewe.

    ReplyDelete
  16. Shigongo ni simu tu au una lingine? sizan kama ni simu na lisura lako baya kama muuza sumu

    ReplyDelete
  17. inaelekea shigo kannyimmwa papuchi na kwa hasira ya kukosa ndio na yeye ana mwasha mtoto wa watu

    ReplyDelete
  18. hadithi na hadthi, hadithi leo, hadithi na hadthi, hadithi taaamu............................

    ReplyDelete
  19. Risiti tu?
    .
    .
    .
    Hapana?
    .
    .
    Luqman Maloto utakuwa unapumuliwa kisogoni.....watoto wa kiume hawana tabia kama hizi. hata kama shigongo ni bosi wako, asikutumie namna hiyo, haujui wamekwaruzana kitu gani.
    .
    .KAMA HUPUMULIWI KISOGONI NA SHIGONGO USINGEANDIKA HAYA...INAELEKEA UNAMUONEA WIVU UWOYA. BADILIKA

    ReplyDelete
  20. Pumbav zenu globo na shigongo wenu, uwoya anawanyima usingizi? Ss hakuna asiyejua umeamua kumchafua kwa sababu zako binafc, km kakunyima papuchi ungetafuta namna nyingine co hii ambayo ht aliokuwa hatujui nn unataka tumejua, be men, kugombana na mwanamke unatuonyesha jinc gn uluvyodhaifu. Na unavyomuandika ndio!
    Kwanza unamuongezea mashabiki

    ReplyDelete
  21. daaaah.....wallah dunia ina mamboo

    ReplyDelete
  22. Noma saaaaanaaaaa

    ReplyDelete
  23. Aaaaahahahahaa shigongo zilipendwaa.. Hunajipya shigongo leave irene uwoya alooone..

    ReplyDelete
  24. Du! Nooooooma kweli!!! nahii ndio TZ nchi nzuri babisa niliozaliwaa ila 2naishi kwa niguse bahati mbaya nikulipizie makusudi yani watawala wababe, wauza unga wababe, matajili wababe, wamiliki wa vyombo vya habari wababe, mgambo wa jiji wababe, makonda wa daladala eti nao wababe, mateja wababe, WANASIASA wababe tena hawa wanatabia yakufanya sisi dalaja la wao kwenda kwenye umaarufu na mafanikio yani nawachukia hawa people any wayyyyyz!! Uzuri wake 2najuana. sasa basi WADAU punguzeni JAZBA milusi mingi humpoteza mbwa. bro Shigongo na tm yako fanya kama hakitokea k2 vile dada angu nawe kausha some tym ligi zinapoteza mda mwachie mungu japo anamengi ya kufanya mana hadi hapa 2shajua nani ni KIBAKI nani RAIRA ODINGA najua kuna wajinga wata DIS......

    ReplyDelete
  25. Pumbavu zenu global! Mnanibania pua juu ya skendo , MBONA HATA HAYO MAPIGA MBWA YENU YANANUKA SKENDO KAMA YAKO CHOON! kwan hatuwajui akina WEMA SEPETU? Umenymwa kitu wewe harafu ni dhaifu mkubwa. Huna lolote global publisher.. UWOYA NAKUKUBALI DADANGU TULIA

    ReplyDelete
  26. Yaan global mnafikir kuandika kwa staili ya kumchamba ni kumsaidia uwoya?? Ndalandefu wa kubwa ninyi futen haraka hii post kabla hamjajiuzuru. Mmetuelimisha nini zaid ya kutuchefua! GLOBAL PUBLISHER HAMFAI KUIFUNDISHA JAMII. Kafien mbali kama mmchoka washenz niny!. UWOYA NAKUKUBALI DADANGU TULIA UCJAR.

    ReplyDelete
  27. mm nna moja 2 mengine na mwachia baba na mama ......hapa TZ ha2na SUPASTAA ata mmoja hii ni kutokana na vigezo vya kiSUPASTAA .....apa tuna MASTAA tu......ukitaka kujua vgezo vya kuitwa SUPASTAA ingia google kaxome....................

    ReplyDelete
  28. Acheni usenge wenu simu na mambo ya mumewe yanawahusu nini mbona bosi weno anawambukiza wanawake ngoma mbona amwandiki mnaliwa kizeri nn

    ReplyDelete
  29. acha ushoga shigongo......!we malaya tu,ukinyimwa unaleta bf nyooooooo!

    ReplyDelete
  30. Shigongo siyo mwandishi wa hizo habari

    ReplyDelete
  31. Hatushawishiki! Irene ni mwanadamu kama watu wengine so kushtak au kushtakiwa ni kawaida sana. Anashtakiwa RICHMOND sembuse Irene! huna jipya Shigongo, umenyimwa UCHI ndo umeona umchafue dada wa watu! nwe, hatujashawishika tafuta mbinu mbadala!

    ReplyDelete
  32. Aisee no mouma

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad