MWANAFUNZI wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kipwa mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa mwenye miaka minane ameweza kujiokoa yeye na mtoto wa dada yake mwenye umri wa miezi mitano kwa kuogelea hadi ufukweni baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye ziwa Tanganyika.
Manusura huyo aliyefahamika kwa jina moja la Prisca akiwa miongoni mwa wengine 15 walinusurika kufa maji ama kwa kuogelea au kuokolewa alipoona mtumbwi huo ukizama, inadaiwa alipiga mbizi majini akiwa na mtoto huyo mchanga mgongoni mwake na kuweza kuogelea kwa saa kadhaa hadi ufukweni wote wakiwa hai.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kipwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyika , Benson Silinjile alithibitisha mkasa huo wa aina yake akisema msichana huyo Prisca alikuwa amempeleka mtoto huyo kupata chanjo katika kituo cha afya kijijini Kapele kwa kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa mgonjwa hivyo alimwomba msaada huo.
Licha ya msichana huyo kuweza kujiokoa yeye na mtoto huyo mchanga kwa kuogelea hadi ufukweni pia nahodha wa mtumbwi huo uliopata ajali hiyo iliyosababisa vifo vya watu 13 wakiwemo wanawake na watoto wenye umri chini ya miaka mitano , Lazaro Sikapote (26) aliweza kuokoa familia yake akiwemo mama yake mzazi Rose Sikapote , mkewe Rakadia Sikazwe na mwanae aliyefahamika kama Nazaro Sikapote.
BINTI WA MIAKA 8 AOGELEA NA KICHANGA HADI UFUKWENI KUJIOKOA BAADA YA BOTI KUZAMA
8
September 28, 2013
Tags
Hii FUTUHI sasa, watu kumi na tatu wafe kenyee ndo kajiokoe na KICHANGA mgongoni wakiogelea zaidi ya masaa..!!!?????
ReplyDeleteHaijaniingia akilini bado njoo kwa staili nyingine.
Sio kosa lako ni kutokuwa na roho ya iman na uelewa wako pia mdogo maana,inawezekana sana kwan hukuona yule mtt kwenye ajal ya mel ya nungwi alivyookolewa anaelea majin huku yeye kalala?
ReplyDeleteAcha ushamba ni kujua tu kuswim at young age ingia YouTube search water babies utakoma na roho yako uone vitoto vidogo vya miezi kadhaa hadi miaka 2 vinavyojua kupiga mbizi na vinageuka kuvuta pumzi halafu vinaendelea utajibeba Kama hujui kuogelea utakufa maji
ReplyDeletemipango ya mungu. kufa kwa wale ickupoteze iman. yakufaa umpongeze kwa ujacli alio nao mtto huyo.
ReplyDeleteJaman achen kudanganyana mtoto wa miaka 8 hawez kuogelea kwa zaid ya saa huku akiwa na mtoto mwingine!!
ReplyDeleteTatizo Wabongo swimming 0 watoto good swimmer kuliko kujifunza ukubwani.
ReplyDeleteINAWEZEKANA KABISA HUYO MTOTO AKOGELEA NA KUJIOKOA NI MAZINGIRA ALIYYAZOEA.MBNA KUNA WATOTO WA MIAKA KAMA HIYO ANAISH MBAGALA HALAFU ANAENDA KUSOMA TEGETA?
ReplyDeleteKWA NINI HUYO MTOTO ASIANDALIWE ILI MWAKA 2020 AKASHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI KULE JAPAN???????????????????????????????????????????????????????ANAWEZA AKAVUNJA REKODI YA DUNIAI. Wewe unayesoma hii comenti hata ukiwekwa kwenye Beseni utakufa.
ReplyDelete