CCM YATOA MIEZI 6 KWA WAZIRI WA ELIMU KUJIUZULU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa kushindwa kulipa madeni ya walimu nchini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pia ametoa muda wa miezi sita kwa Waziri huyo na Naibu wake Philip Mulogo kutekeleza hilo agizo hilo vinginevyo chama kitawatumia wabunge wake kuwatimua kwa nguvu.

Kwa mujibu wa taarifa za madeni zilizokusanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), hadi sasa walimu wanadai malimbikizo yao ya Sh bilioni 49 ambayo hajalipwa na Serikali.

Kinana alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara jana katika wilaya za Bariadi na Busega.

Alisema CCM haiko tayari kuona walimu wakinyanyaswa wakati wana madai ya msingi.

Hivi sasa imejengeka tabia kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa wizara ya kuwadharau walimu na hata kuwanyanyasa huku wengine wakishusha utu na heshima ya walimu kwa kuwatukana, alisema.

Kinana ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa alisema kwa mawaziri kushindwa kutatua kero za walimu, imefika wakati wahusika waondoke wenyewe na wasipofanya hivyo chama kitawaagiza wabunge wake wawafukuze kwa nguvu.

“Ninatoa muda wa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wakiwamo watendaji kuhakikisha wanalipa madeni ya walimu haraka. Haiwezeni hii ni nchi ya watu wote wakiwamo walimu wadharauliwe na hata kunyanyaswa kwa maneno ya matusi

Hili hapana CCM haiko tayari kuona walimu kila siku wakipigwa danadana kutokana na uzembe wa watu waliokabidhiwa dhamana za kuongoza sekta ya elimu katika nchi yetu,” alisema.

MTANZANIA ilimtafuta Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ambaye alisema hadi sasa madeni ya walimu yamefikia Sh bilioni 49 ambayo ni malimbikizo ya mishahara na mapunjo.

Kila mara tunawaambia kuwa ni vema Serikali itafute Sh bilioni 100 katika fungu la dharura ili iweze kulipa madeni ya walimu na iachane nao lakini hawasikii,” alisema Oluoch.
SOURCE MTANZANIA
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. That's BIG RESULTS NOW

    ReplyDelete
  2. Angalau kidogo CCM mmeongea kapoint.

    ReplyDelete
  3. Wanajikosha tu hawana lolote wanajua2015 walimu ndiyo wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, wanafki wakubwa.

    ReplyDelete
  4. Wanajikosha tu hawana lolote wanajua2015 walimu ndiyo wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, wanafki wakubwa.

    ReplyDelete
  5. Ha! Kumbeeeeee. Nimejua janja yao. Hapo wamenoa.

    ReplyDelete
  6. danganya toto hiyo ,leo ndo limeonekana hilo? walim toka enzi wanasota katka hal ngum vijjni na vijishahara vyao,ila si mbaya mkiwakumbuka kwa kumaanisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uncle Samy Singida .CCM inafanana na mwanaume mgomvi na mwongo anae mpiga mmke wke afu ucku anataka MECHI YA UTAMU co ndo maana 2015 imekaribia wajua ni mech ya utamu na walimu ndo wahucka miaka mingi mnawanyanyasa walm. Hyo ni sawa na kumwambia mkeo nakuletea WAX afu kumbe umefunga kachupi kwnye rambo. KINANA hpo bado hyo c sela sbrn 2015 mnyolewe DONGO kama umekelwa nitokee0767724328

      Delete
  7. labda wanafikiri walimu niwajinga kiasi hicho cha kuwachezea, kuwadharau na kuwaona ni wepesi wa kusahau. ccm umefika mwisho wenu! FREEDOM IS COMING TOMORROW...! ALUTA CONTINUE....!!!!

    ReplyDelete
  8. wewe kinana wewe acha cinema wewe unajua kabisa shukurukawambwa nibinam wa boss wako hata ukimpa miezi miwili unajuhakunakitakacho fanyika.na wewe there is nothing u can do naunajuua ukimkomari kawambwa hata. huo ukatibu mkuu ulionao utatimuliwa. unakumbuka kwenye kampeni za jk 2005 ulikua kampeni manager wa jk.baba na mwana walikufanya je jipange. m.ng.machimkenda.

    ReplyDelete
  9. poleni waalimu mkae mkijua 2015 ndio hiyoooo lazima msimamie uchaguzi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad