DAKTARI FEKI AKAMATWA AKIHUDUMIA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI

DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
  
‘Daktari’ huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.
Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.

Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari .

Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.

Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.

Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.

Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.

Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.

Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali. Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.

Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.

Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.

Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.

Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.

“Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi,” alisema.

Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa ‘Masters of Medicine’, ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.

Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.

Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

-Habari leo

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Each and every thing in this KANTIRI IZ FEKI..!!! Even DAKETARE Mmmh mai wasu mtatuuwa wejasuuu Mungu chisakilye!!! ai bhutakaaaa!

    ReplyDelete
  2. Wewe hujaeleweka bchwa alaahh, jaman inackitishaa sana afu huyo atateswa na kupata adhabu kalii wkt wauza sembe wanaachiwa kiurahic huko sheeennzzzzzz

    ReplyDelete
  3. Huu ni uzembe wa management ya muhimbili.au wa HR au katibu wa hospitali.nainamaana hamna briefing yakilasiku ya madakitari au hakuna vikao vya madakitari.acheni cinema. mlikuamnamjua sana inawezekana alikuwa anawasaidia sana ktk kuchukua rushwa hamnalolote mekalia rushwa tu.m.ng.machimkenda

    ReplyDelete
  4. OMG!!!!namjua huyu kaka jamaniii...uwiiii na amekuwa akinisaidia saana nikiwa na matatizo ya kimatibabu,noo....Dr Macha kumbe sio Dr?????hapana jamanii...Namjua nimeanza kumuona muhimbili tangu 2010 nimejifungua na anakuja anaingia hadi labor na manesi wote wanamwita Dr,hapana kweli huu ni mchezo unaofahamika na uongozi...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisaaaa,lakini atakavyopelekeshwa na mapolice,agness masogange wamemuachia,Nina hasiraaaa mpaka nangata meno.

      Delete
  5. Wamuache miaka Mia moja Kama walivyomuacha agness masogange.

    ReplyDelete
  6. hii ndio bongo ukikamatwa shauri yako tusitajane

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad