DR SLAA:LAZIMA WABUNGE WATANDIKANE MAKONDE NDANI YA BUNGE ILI HESHIMA IWEPO

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema tukio la kupigwa ngumi na askari ndani ya Ukumbi wa Bunge lilisababishwa na amri ya Naibu Spika, Job Ndugai na wala siyo askari.

Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai askari.

‘Sugu’ alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo ziarani mkoani Mbeya wakifanya mikutano na wananchi kwa lengo la kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na wabunge wengine bungeni hivi karibuni.

‘ Sugu’ alidai kuwa Ndugai ni adui wa wapinzani bungeni na kwamba kwa vyovyote vile ilikuwa vigumu kuvumilia kwa mtu yeyote baada ya askari kuanza kupiga wabunge kutokana na amri ya Ndugai.

Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema kitendo alichofanyiwa Sugu hakikuwa kibaya kwake peke yake, bali hata wananchi waliomchagua.

Hata hivyo, Dk Slaa alisema kwa upande mwingine ili heshima ya Bunge lolote lile duniani iwepo, ni lazima wabunge watandikane makonde ndani ya Bunge na si vinginevyo hivyo hashangai kwa kilichotokea kwa Sugu bungeni.

Dk Slaa, alimjia juu Ndugai akisema alikiuka Kanuni za Bunge kwa kitendo hicho na kubainisha kwamba kanuni za Bunge zipo wazi kabisa kwamba iwapo itatokea vurugu ndani ya Bunge anachotakiwa kukifanya ni kuahirisha Bunge kwa wakati huo.

Pia alisema askari ambao ni wapambe wa Bunge ‘Sargent at arms’ ndio wenye mamlaka ya kuingia ukumbini na endapo itatokea nguvu ya ziada hao ndio wanaotakiwa kisheria na siyo kuwaita askari wa nje ya Bunge kuingia ndani.

Dk Slaa alisema kitendo kilichofanywa na Sugu pamoja na wabunge wengine ni cha kijasiri na aliwataka kutokurudi nyuma na misimamo yao bali waendelee kusonga mbele.
Chanzo: Mwananchi.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nawapa pongezi makamanda hakunakulala mpaka kieleweke.m
    ng machimkenda

    ReplyDelete
  2. Huyu babu inaelekea ana ugonjwa unaitwa [UWAKI[ UKOSEFU WA AKILI KICHWANI halafu anaitwa babu anasema maneno ya vijiweni anakosihi huko stakishali

    ReplyDelete
  3. Mpumbavu huyu hafai hata ujumbe wa nyumba kumi, Sa hii
    Inatofautiana nn na kauli aliyotoa pinda kua wapgen 2mechoka??? Acheni mc2lee uxenge hii nch ni ya watz

    ReplyDelete
  4. ,unamtukana dr.slaa kwa maslahi ya nani wewe mbururula? Kama wewe ni ccm endelea tu kupiga punyeto zenu,dr.ikulu ataingia tu.

    ReplyDelete
  5. hakuna mweny uchungu na nchi hii zaidi ya kujishaua na kutafuta maslahi.
    undeleeni kutoka manundu umaarufu hauji bila skendo.
    MAKAMANDA WAOGA.

    ReplyDelete
  6. ataingia kwenda kuwaona au kuwasalimia wenzake na si kwa post ya uras

    ReplyDelete
  7. LAZMA WABUNGE WATANDIKANE. Yan we mzee na akil zako ndo kweli uwezo wako wa kufkil umeku2ma kutoa kauli hii? Unaleta picha gn kw watz?? C mnaoneka mnafanyafanya usenge 2. Sa ungekua ndo rais cjui ungetoa kauli gn!! Kuma kibuyu.

    ReplyDelete
  8. Hahahaaa!! Hiii ndo tz aka afrika bhana wa2 wanatafta kula sio kura. Hakuna demoklasia huku dunia ya3. Wote wezi 2 ngoja wakipewa nafac ndo utajua. Madafakaz..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad