Prince Dully Sykes amesema anamfananisha hitmaker wa ‘Number 1’ Diamond Platnumz na marehemu Steven Kanumba kwa jinsi alivyo na moyo wa kuthubutu katika mambo yake.
Dully Sykes alikuwa akiongea na Bongo5 kwenye uzinduzi wa video ya video mpya ya Diamond uliofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Diamond ni namba moja kwasababu yupo tayari kujitoka kwa kila kitu,” alisema Dully. “Naweza kumfananisha Diamond na mtu kama Kanumba. Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.”
Pia Dully amesema mwishoni mwa mwaka huu anatarajia kuiongezea vifaa vipya studio yake ‘4.12’ ili kujiimarisha zaidi kwenye utayarishaji wa muziki ambao anasema kwa sasa anaufurahia zaidi kuliko hata kuimba.
hakuna lolote
ReplyDeleteHebu tutolee ushuz hp
ReplyDeletekhaa wabongo hapo juu si lazima mcoment
ReplyDeleteDiamond afanane na Kanumba? Haiwezekani na haito kuwepo then mbona wimbo wenyewe wa Diamond ni wakawaida saaaana binafsi sijaona ubunifu wowote pale
ReplyDeleteMaskini ambao hamna hata hela za kubadilisha mboga unakaa kumponda m2 anayefanya yake mbwa nyinyi fanyen yenu na nyinyi achen miwivu ya kisenge Diomond anafanya yake!
ReplyDeletembona mambo kama haya AY alishafanya
ReplyDeleteKwel bhan mwachen Diamond afanye yake cz yupo juu nw dayz.
ReplyDeletejmn kama hujisikiii kucoment acha as long as jamaa kazi anajitahidi tusiwe wanafiki ndomana wabongo hatuendelei 1love diamond kazi nzuri komaaaaa
ReplyDeleteWachawi na wangaa hawana nafasi bhana big up
dogo anatisha wenye roho mbaya kawaida yao kuongea hovyo.
ReplyDeletekiukweli Diamond mnamsifia bure wala hawezi fanana na kanumba kwani anajitapa kwa kujiona na kuhusu daz nunda nampa pole sana na MUNGU AMPE HALI NJEAMA NA AWE SAWA AMEN.
ReplyDelete