HIVI NDIVYO WAFUASI WA RAIS ASSAD WA SYRIA WANAVYOUAWA MBELE YA WANANCHI

Askari wa kundi la ISIS akimwekea jambia shingoni mmoja wa wafuasi wa Bashir al-Assad kabla ya kumkata kichwa.
Baadhi ya mateka wanaomuunga mkono Rais wa Syria, Bashir al-Assad, wakiwekwa eneo la machinjioni.
Mmoja wa askari akiinua juu jambia kumkata mfuasi wa Bashir al-Assad.
Mtoto mdogo raia wa Syria akiangalia mwili wa mfuasi wa Bashir aliyekatwa shingo.
Watoto wakishuhudia mwili wa mfuasi wa Bashir aliyekatwa shingo.
Baadhi ya mateka wakisubiri kuuawa.
WATU wanaomuunga mkono Rais wa Syria, Bashir al-Assad, wamekuwa wakikamatwa na kuuawa mbele ya wananchi.  Mauaji yamekuwa yakifanywa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukatwa shingo au viungo vya mwili kwa kutumia majambia na silaha zingine.
Haya yote hufanyika  mbele ya watu wanaoshangilia na wengi wao wakiwa na silaha. Miongoi mwao ni pamoja na watoto.  Mauaji ya mwisho ambayo yalinaswa hivi karibuni ni yale yaliyotokea katika mji wa Keferghan kaskazini mwa nchi hiyo.
Inasemekana mauaji hayo hufanywa na kundi la ISIS ambalo ni tawi la Al-Qaeda linalompinga Assad na wanaofanyiwa mauaji hayo ni kundi linalojulikana kama Shabiha (Mizimu) ambalo linamuunga mkono rais huyo.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Maandiko ya BIBLIA yanatimia

    ndugu watauana wenyewe kwa wenyewe

    tukeshe tukisal kwan hatujui saa wala dakika

    ReplyDelete
  2. inatia uchungu sana mola atuepushe na majanga zaidi

    ReplyDelete
  3. mh inatia huruma sana,,,,mungu awasemehe!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Hao wanaowaua wenzao hawajitambui,kwani hata wao hawataishi milele,pia hawajui chuki wanayoirithisha vizazi vijavyo,wasijidanganye kuwa watakuwa na nguvu siku zote.

    ReplyDelete
  5. Kumbuka auae kwa upanga naye atakufa kwa upanga

    ReplyDelete
  6. mmmmh siku zimekaribia,

    ReplyDelete
  7. Bora utubu makosa mapema usije kuhukumiwa na hao wauaji. Siku za kurudi kwa Yesu Kristo zi karibu. Kuwaua ndugu zako.....

    ReplyDelete
  8. Obama na washirika wake wako wapi.mbona aya yanayotokea awaoni

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad