JE! ILIKUWA SAHIHI KWA DIAMOND KUMNUNULIA GARI YA KWANZA MZEE GURUMO?

Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado ya kawaida sana na hakuwahi hata kumiliki gari toka enzi hizo' niliona kuna kitu hakiko sawa... sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile 'atakuwa alichezea maisha ujanani'

Siku si nyingi  tulioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali. Wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...

Mfano: Mzee Gurumo  alisema alilipwa 'elfu ishirini' mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani? Na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka huo 1978... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa 'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne' na alikufa bila nyumba wala kibanda..

Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu, Wajomba, babu na kadhalika ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe.... utasema hawakupata chochote ujanani kumbe anasa, starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....

Ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama mara watoto, mara serikali na kadhalika....

Huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond... angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...Am just Thinking Aloud tu kwasababu nimeanza kusikia umaarufu wa huyu Mzee katika Music Toka Nizaliwe Hajawahi Kuchuja.....
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Napenda saana watu wanaoleza ukweli kama hivi,nivizuri kwenye mapungufu tuweke wazi ili tujifunze kupitia mapungufu ya waliotutangulia,kuna watu maarufu wanakufa kwa madawa ya kulevya lkn hazitolewi taarifa sahihi ili jamii ijifunze,kiukweli hata kama mziki hauli

    ReplyDelete
  2. Kweli atakuwa alikalia starehe

    ReplyDelete
  3. yote hayo matazamio tu ya watu lakini mi nahisi ingekuwa bora zaidi mzee mwenyewe angesema kwa nini hakununua gari, coz nyumba anayo so yawezekana hakuwa na mpango wa kununua gari katika maisha yake 7bu hujui mipango ya mtu binafsi...............

    ReplyDelete
  4. sio lazima ununue gari. nyie mnaweza kumuonea huruma kumbe mshkaji anapenda kutembea zaidi;

    ReplyDelete
  5. Kweli Gurumo awe ni fundisho kwa wasanii wanaojirusha ujanani bila kutambua kuwa fainali ni uzeeni.

    ReplyDelete
  6. Kwa hiyo hutaki au?
    Hizi ndo tunaziitaga jilaz za kifalafala. au ulitaka upewe wewe? Swala la kwamba ametumiaje pesa ujanani mwake hilo halikuhusu pumbavu yani tena huna adabu kabisa mwone kwanza

    ReplyDelete
  7. ACHENI KUTUMIA MUDA WENU MWINGI KUDISKASI MALIYOPITA,NI UJINGA!!! MZEE NGURUMO KUPEWA GARI ISIWE NDO MADA YA KILA SIKU KUJADILIWA,KUNA MAMBO MENGI YA UMUHIMU YANATUKABILI NA YANAHIJIWA KUZUNGUMZWA KWA MAPANA.....MNASHINDWA KUTUMIA UWEZO WENU WA KUFIKILI KULINGANISHA MASLAHI YA MZIKI WA ZAMANI NA WA SASA? WA ZAMANI HAUKUWA NA PESA KAMA SASA,,,MBONA NYINYI HAMJUTIII PESA ZENU KULIPIA TIKETI KUINGILIA TAMASHA AU MUZIKI? KWANI KUINGIA MZIKI NI LAZIMA? UNGEKUWA MNAJALI HIZO PESA SI MNGENUNUA HATA SUKARI MKAPELEKA KWENYE VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA MPATE DHAWABU KWA MUNGU? DIAMOND YUKO SAHIHI KABISA,NA WALA SI KWAMBA ANA MIHELA MINGI SANA KULIKO WATU WOTE ILA NI KUJALI WENGINE WANAOHITAJI ZAIDI!!!!!!!!!!!!!! TUBADILIKIENI JAMANI eeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad