JE TANZANIA NI TISHIO KWA NCHI ZA EAC KIUCHUMI-MBONA YAPIGWA VITA NA VIJEMBE NA NCHI ZINGINE?

Wiki iliyopita ulifanyika mkutano Mjini Mombasa na kuhudhuriwa na marais, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Salva Kiir wa Sudan Kusini,  lakini Rais Kikwete hakuhusishwa.

Tangu Rais Jakaya Kikwete alipotoa ushauri kwa nchi ya Rwanda kukaa na waasi wa FDLR ili wamalize migogoro yao, uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umekuwa shakani.

Uhasama huo unatokana na Kundi la M23 linaloundwa na wapiganaji wa Kitutsi likiaminika kusaidiwa na Rwanda na linapambana na majeshi ya Serikali ya DR Congo. Hata hivyo, Rwanda inapinga kuisaidia M23.

Kumekuwa na malumbano kupitia vyombo vya habari vya nchi hizo mbili huku kila upande ukirusha vijembe vya kumponda mwenzake.

Mbali na vijembe, hivi karibuni Rwanda imejitoa na kuanza kuacha kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuingizia mizigo yake, badala yake sasa imejielekeza Mombasa nchini Kenya.

Hali hiyo inaonyesha kuiathiri Tanzania hata katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo katika mikutano ya hivi karibuni ya wakuu wa nchi hizo, Rais Kikwete hakushiriki.

Mkutano huo uliofanyika wiki iliyopita mjini Mombasa na kuhudhuriwa na marais, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Salva Kiir wa Sudan Kusini walialikwa na kutuma wajumbe wao, lakini bila kumhusisha Rais Kikwete ni moja ya dalili ya Tanzania kutengwa au kuenguliwa.

Baada ya mkutano huo, marais hao wamezindua eneo jipya la bandari ambalo litasaidia kuimarisha huduma ya kupakia na kupakua mizigo.
Serikali ya Kenya imesema ujenzi wa sehemu hiyo mpya umefanyika kwa kutumia kipato cha ndani bila msaada wowote kutoka nje.



Mkutano huo unafuatia ule wa mwezi Juni uliofanyika mjini Kampala, Uganda ambao pia Rais Kikwete hakualikwa.



Katika mkutano huo ilikubaliwa kwamba, nchi za Afrika Mashariki zipunguze gharama za usafirishaji bidhaa kwa kupanua usafiri wa reli pamoja na kuboresha huduma za bandari, hususan ile ya Mombasa sambamba na kuharakishwa ujenzi wa bandari kubwa visiwani Lamu.



Kutokana na hali hiyo, Tanzania sasa imemwomba Rais Museveni wa Uganda kuisuluhisha na Rwanda.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh hapa ni kitendawili. Sasa museven atasuluhishaje wakati ndiye anayeshirikiana na Kagame kuitenga Tanzania?

    ReplyDelete
  2. Hao washenzi wa hizo nchi wanaona wivu tu jinsi jk anavyopasaua mbuga na kutembelewa na viongozi wakubwa duniani, na kagame ndo leader wao, watarudi wenyewe nn kuwabembeleza.

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani serikali yetu ya Tz ina kazi kubwa ya kutueleza ukweli wa nini kinaendelea,maana ni kujidhalilisha kutokana na historia ya nchi yetu,utajiri wetu,na ukubwa wetu kwenda kuomba kupatanishwa na Rwanda,pili nadhani kuna siri kubwa imejificha zaidi ya hiyo inayosemwa ya M23,kwahiyo serikali ituambie ukweli,isitoshe mini naona hawa jamaa kama wanafaidika na Tz katika hii EAC Yao.

    ReplyDelete
  4. No need kwan hatupo kwenye integration nyingne?otherwise kuwe kuna kitu nyuma ya pazia. Na hao nao watuumize kichwa?madn tunayo,ges tunayo, mafuta yapo, vivutio bwerere we can jaman ila waliopewa dhamana ndo wanatuangusha

    ReplyDelete
  5. Upumbavu,kwani,watizi,2naish,kwakutegemea,rwanda,sizani,hiro,tanzania,ijitoe,eac,

    ReplyDelete
  6. Mnaongea pumba watanzania na hamna chenu mnategemea kenya kwa sana. Subiri mtengwe muone ngoma yenyewe...nkt!

    ReplyDelete
  7. Ni kweli rasilimalu ziko tele ni viongozi tu wanatuangusha. Lait kama wangekuwa hawali rushwa na kujilimbikizia mali kila mtanzania angekuwa walau na pikipiki. Mungu tusaidie.... tuhurumie. Tuombee nchi yetu jamani. Viongozi wamwogope mungu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad