KINA DADA AMBAO HAMJAOLEWA.HEBU FUNGUKENI HAPA!

Inasemekana Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia. Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.
Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu.
Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote. Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi. Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa.
Girls mfunguke ni kweli haya
Tags

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umekariri. Uongo mtakatifu huo..m
    Wanawake kwa sasa tunajiamini sana, tunatafuta maisha mazuri kuliko kufikiria kukimbilia kuolewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We acha uongo hp unatamani kuolewa na kuwa na familiya yako hy wengi husema mdomoni kuwa hawana haja ya kuolewa wala hawana mpango ila in reality unataman sana uolewe sema hampendi kukiri ukwl wa mambo moyon unaumia kujiuliza we mbn umri unaenda uzuri unao tatizo ni nin ila mbele ya watu ndio unatoa maneno hy

      Delete
    2. Kwani ww uliolewa kwa uhodari wako?

      Delete
  2. Kuolewa kitu gani. Watu tuna malengo kibao tukimbilie kuolewa. Hata miaka arobaini mtu anaolewa sembuse twenty five!
    Usituchoshe babu ww

    ReplyDelete
  3. Anonys hapo juu waongo wakubwa na kma ni wasichana wa umri huo hamjielewi nenden mkaombewe au msomewe dua.ni kweli kabisa msichana akifka 25 akili inaanza kumkaa sawa kidogo kma ana mambo ya ajabu anaanza kuacha ilu apate mume akifka 27 ndo anakuwa na hamu ya mume na watoto wasichana mcjidanganye hata kama una pesa kiasi gani na unajiweza kwa vyote huwa tunataman tuwe na wenza wetu wa maisha.na mwanamke bila mume haheshmki.mimi nina kila kitu nilichokihtaji kwa muda huu na age niliyokuwa nayo ila sasa hvi huwa nasema chitaji kingne kwa sasa zaid ya mume na mtoto hata nikifanya kaz cfanyi kwa raha coz najua hamna anaenizunguka na ninafanya kwa ajli ya nani.girls achen ujinga

    ReplyDelete
  4. Kweli mtupu nampa bgup huyo wa juu kwa maneno yake ya ukweli,wasichana wenye umri huo uwaza sana kupata mtt na kuolewa.

    ReplyDelete
  5. Mfano hai ni wadada wa clouds ambao hawajaolewa. Kwani hamuwaoni?????

    ReplyDelete
    Replies
    1. True mdau,wadada wa clouds na hata mastaa wetu wa bongo ambao hawajaolewa wanahahah kila siku kufaiti ili waolewe.dat ukweli kabisa.mfano hai ni mm mwenywe nimekuja kuwa na mtoto na mtu ambaye hata hadi leo najiuliza yalinipataje hadi kufika kwake sijui hadi leo I waz 27,so its very true mdau

      Delete
  6. Sio kweli, labda wanawake wa kiafrica ndo wanatabia hiyo, ila wazungu kuolewa wala sio issue kwao.wanapenda sana kuishi kama gal frnd/boyfrnd kuliko kuoana

    ReplyDelete
  7. kuolewa sio deal sana sikuhiz ilikuwa zan zaidi ni.kujitafutia mateso wadada tafuteni mahela kila kitu kitakuja okeee??

    ReplyDelete
  8. kuolewa sio deal sana sikuhiz ilikuwa zan zaidi ni.kujitafutia mateso wadada tafuteni mahela kila kitu kitakuja okeee??

    ReplyDelete
  9. sio kweli. mimi nawafahamu wadada wengi wenye umri zaidi ya miaka 40, wala hawafikirii kuolewa. Bado wanavaa, cheza, imba kama Rihanna, wanajiona watoto wakati wana nywele nyeupe kule mahala. wamegoma kuzeeka.

    ReplyDelete
  10. Ila kam umri umeenda, hujapata mtoto, zaa hata katoto kamoja tu, mume umekosa, na mtoto pia,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad