KINANA"SEREKALI TATU TANZANIA NI HATARI-TANZANIA ITAISHANGAZA DUNIA"

*Aonya zitasababisha machafuko 
*Asema Tanzania itashangaza dunia
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendeleza msimamo wake wa kupinga muundo wa Serikali tatu kuingizwa katika Katiba mpya, kikisema kuwa muundo huo ni hatari kwa umoja na mshikamano wa taifa.

Chama hicho kimeonya kuhusu muundo huo na kusema kuwa Serikali zaidi ya mbili zinaweza kuvuruga ustawi wa taifa, kwani ni rahisi zaidi nchi kuingia katika machafuko.

Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini.


Kinana alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa na kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na marais watatu, jambo ambalo halipo duniani kote. 

“Katiba ni jambo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu, lakini katika hili la kuwa na Serikali tatu ni hatari, kwani kwa mujibu wa rasimu yetu ya sasa, inaonyesha kuwa kila Serikali itakuwa na mamlaka kamili.

“Ikiwa kutatokea serikali moja kati ya hizo tatu na moja ikasema sasa inanunua vifaa vya kujilinda, basi ile ya Zanzibar nayo itafanya hivyo na ile ya Muungano pia itafanya hivyo.

“Hata kama kuna vita serikali moja ikasema hatutaki nyingine itasema tunataka, mwishowe mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kinana na kuendelea: 

“Kwa hali hiyo, ninachotaka kuwaambia ni kuwa Katiba Mpya itaandikwa na maisha yale yale yataendelea. Afrika Kusini, India na Kenya wamebadili katiba zao, lakini hali ya maisha ya wananchi wao iko vilevile,” alisema.

Katika mkutano huo, Kinana alisema msimamo wa chama chake kuhusu muundo ni Serikali mbili na kueleza kuwa chama chake kitaheshimu maoni ya Watanzania kuhusu muundo wowote bila shinikizo la kisiasa.

Alisema hatua ya kuwa na wingi wa Serikali kuna hatari ya nchi kuwa na Bunge la Mabwenyenye na Bunge la Makabwela, ambapo alisema kuna hatari ya fedha za walipa kodi kutumika vibaya.

Kinana alionya hatua ya kuwa na ukubwa wa Serikali ambayo itakuwa mzigo kwa Watanzania, ambao wamekuwa wakiendesha kwa kulipa kodi zao.

“Hivi sasa nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa CCM itakuwa tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayoamuliwa na wananchi.

“…. Na ikiwa mtaamua kuwa ya Serikali mbili, tatu hata tano sawa, lakini kubwa katika hili CCM hatuhitaji mchakato huu ufanyike kwa kuingiliwa kwa shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani au hata taasisi ambazo zimejificha kwa mlango wa nyuma.

“Sisi tulisema wazi tunapenda tuendelee na Serikali mbili, lakini katika hili tambueni kuwa na Serikali nyingi zaidi kuna hatari ya kuingia katika mifarakano na hata vita,” alisema Kinana.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua ya baadhi ya watu kupita na kupandikiza chuki kuhusu Katiba Mpya, mawazo yao yanatakiwa kupimwa, kwani watu hao wana lengo la kuvunja badala ya kuimarisha umoja.

“Ni muhimu kuandika Katiba mpya ambayo itasaidia kuweka misingi bora na imara ya uongozi, lakini si kuwa na Katiba yenye utitiri wa kila aina ya Serikali, hili hapana, ila ikiwa mtaamua nyie wananchi wenyewe sisi hatuna pingamizi,” alisema.

Mapema Agosti mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, aliwataka wanachama wa CCM kujiandaa kisaikolojia na muundo wa Serikali tatu, ikiwa Watanzania wataamua hivyo.

Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari kupitia vikao vya NEC mjini Dodoma, ambapo alisema mwaka 1992, kundi kubwa la wananchi lilipinga kuingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini lilisikilizwa na nchi ikaingia kwenye mfumo huo.
Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ninamuunga Mkono Mh. Kinana kwa mtazamo wake.

    ReplyDelete
  2. nyie CCM msiwafanye wenzenu wajinga waoneleeni huruma,kazi yenu kuwatisha na vita na gharama za uwendeshaji wa hio serikali.wakati ikiwa mambo mengi yashaondoshwa katika mambo ya muungano, mtaogopa mpaka lini nyinyi wabara kujitegemea wenyewe mnataka kuwanyonya wazanzibar mpaka lini,mbona wazanzibar wao wana derikali yao muda mrefu wao hawaogopi gharama?au hamtaki hizo serikali tatu mnaogopa kulirudia jina lenu laTanganyika mnataka kuendelea kuwakandamiza wa zanzibar lini mkae mkijuwa wazanzibar hawautaki tena huo muungano wenu wa kitapeli wanachokitaka ni nchi yao,na washasema hawapokei lolote pungufu zaidi ya mamlaka kamili na hiyo ccm yenu haipo tena huko ZANZIBAR.,amebaki Borafia na Sadifa je mtauweza umma wa Zanzibari na washavinjari kudai nchi yao kutoka kwa wakoloni weusi nyie watanganyika

    ReplyDelete
  3. nyie CCM msiwafanye wenzenu wajinga waoneleeni huruma,kazi yenu kuwatisha na vita na gharama za uwendeshaji wa hio serikali.wakati ikiwa mambo mengi yashaondoshwa katika mambo ya muungano, mtaogopa mpaka lini nyinyi wabara kujitegemea wenyewe mnataka kuwanyonya wazanzibar mpaka lini,mbona wazanzibar wao wana derikali yao muda mrefu wao hawaogopi gharama?au hamtaki hizo serikali tatu mnaogopa kulirudia jina lenu laTanganyika mnataka kuendelea kuwakandamiza wa zanzibar lini mkae mkijuwa wazanzibar hawautaki tena huo muungano wenu wa kitapeli wanachokitaka ni nchi yao,na washasema hawapokei lolote pungufu zaidi ya mamlaka kamili na hiyo ccm yenu haipo tena huko ZANZIBAR.,amebaki Borafia na Sadifa je mtauweza umma wa Zanzibari na washavinjari kudai nchi yao kutoka kwa wakoloni weusi nyie watanganyika

    ReplyDelete
  4. hivi watu mnavyopiga kelele Zanzibar inanyonywa? inanyonywa nini? nachoota Zanzibar ni utalii tu, other than that sioni kingine, Tanganyika huo utalii upo, madini yoote yako bara? kilimo kikubwa kiko bara, sana sana Zanzibar ikisimama peke yake, mtaend up kutawaliwa na waraabu tena. jamani mtoto akililia wembe mpe

    ReplyDelete
  5. msitutishe tunaweza wazanzibr ilikuwa si nchi maskini umaskini umekuja baada ya muungano,nyie watanganyika ndio mlotutia ufukara

    ReplyDelete
  6. msitutishe tunaweza wazanzibr ilikuwa si nchi maskini umaskini umekuja baada ya muungano,nyie watanganyika ndio mlotutia ufukara

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe unaota, ungekuwa karibu ningekupiga kibao ili UAMKE!!!

      Delete
  7. Dunia nzima hamna muungano wa aina hii.msiwafanye wazanzibar madubu

    ReplyDelete
  8. Mhhh mhh wazanzibar walivyo wavivu mxiuuuu mpaka kuku mna import alafu mnasema muungano unawanyonyaa hamuoni hata aibu

    ReplyDelete
  9. Hivi kwani hao wazanzibar wanafikiri tunafaidika nn na huo muungano?eti tunaogopa kuitwa watanganyika yaani hiyo nayo mnaona ni sababu pumbavu kweli, kwa taarifa yako wanaolinda huo muungano ni viongozi wa ccm siyo sisi wananchi,wala hatutaki huo muungano wenu na hutupati faida yoyote na huo muungano na hatuna tabu kuitwa watanganyika, kwa hiyo tulia na nenda kanywe kahawa, na mlivyojazana karikoo tutafukuza wote pumbafu kabisa.

    ReplyDelete
  10. Hivi kwani hao wazanzibar wanafikiri tunafaidika nn na huo muungano?eti tunaogopa kuitwa watanganyika yaani hiyo nayo mnaona ni sababu pumbavu kweli, kwa taarifa yako wanaolinda huo muungano ni viongozi wa ccm siyo sisi wananchi,wala hatutaki huo muungano wenu na hutupati faida yoyote na huo muungano na hatuna tabu kuitwa watanganyika, kwa hiyo tulia na nenda kanywe kahawa, na mlivyojazana karikoo tutafukuza wote pumbafu kabisa.

    ReplyDelete
  11. Wananzibar si wavivu wamejaa dudia nzima wala hawatishwi na kufuzwa kariakoo,kariakoo kitu gani wako new york mpaka washington manchester mpaka liverpool huko wanakunywa kahawa?hapana niwafanyaji wakazi nyie ndio wezi watanganyika, hupenda utajiri wa harakaharaka,kuungana na watanganyika imekuwa balaa air port zote duniani wameziharibu kwa madawa ya kulevya tukiwaambie hatutaki mnatungangania nini,muungano kwa kwa nguvu,kaunganeni na Uganda,malawi washenzi wenzenu,pamoja na watwana wengine

    ReplyDelete
  12. Wananzibar si wavivu wamejaa dudia nzima wala hawatishwi na kufuzwa kariakoo,kariakoo kitu gani wako new york mpaka washington manchester mpaka liverpool huko wanakunywa kahawa?hapana niwafanyaji wakazi nyie ndio wezi watanganyika, hupenda utajiri wa harakaharaka,kuungana na watanganyika imekuwa balaa air port zote duniani wameziharibu kwa madawa ya kulevya tukiwaambie hatutaki mnatungangania nini,muungano kwa kwa nguvu,kaunganeni na Uganda,malawi washenzi wenzenu,pamoja na watwana wengine

    ReplyDelete
  13. Ni tanganyika si tanzania bara.

    ReplyDelete
  14. shoga la kisomali kazi kudanganya watu unafikiri watu watakuwa wajinga siku zote?

    ReplyDelete
  15. shoga la kisomali kazi kudanganya watu unafikiri watu watakuwa wajinga siku zote?

    ReplyDelete
  16. Kwani kuna tatizo gani tukiwa na serikali ya tanganyika.

    ReplyDelete
  17. Tuache tupumue hatuuutaki muungano wazanzibari tushasema.. Ebu fikirir asilimali za zanzibar zinawekwa kwenye muungano lkn za tanganyikza hazipo kwenye muungano mambo haya vipi jamanii.. Mnatuibia kweupe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad