Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa mpaka sasa ni kama milioni zaidi 150 zinahisiwa kuibiwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo hilo amesema matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga upya.
Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili T220 AMV na kuondoka nao kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Hao wafanyakaz wa hiyo Bank watakuwa wanajua kinachoendelea.Alafu pia inashangaza,huyo jambazi aliyevalia sare za police kazitoa wapi kama si police wenyewe kujihusisha na uhalifu?
ReplyDeleteThis is too much now
ReplyDeleteHalafu mnakaribisha wawekezaji, kuna nchi huwezi hata siku moja ukasikia mlio wa risasi.hata watalii hawawezi kuja huko, hakuna amani
ReplyDelete