MATANUZI YA KUFA MTU.., KUMBE ILIKUWA JEURI YA MADAWA YA KULEVYA

Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa kujibana ajabu, cha kushangaza naenda kujionea jinsi watu wanavyojirusha kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya mavazi waliyovaa ndio usiseme.

Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje? Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA! 

Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa.... naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub, magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha maana tutasikia hata tusiyoyatarajia.....

WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh! Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee mateja yanavyonesa ..... balaa hili. 

EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO CHA MENDE, WATOTO WETU WAPONE; AMENI.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Its all in the mind, if you unconsciously have a belief against money, you will never have it until you find out what the belief is and trully change it!

    ReplyDelete
  2. Kwa hii trend ya wanaokamatwa na madawa tena basi ni wale punda tu na walikuwa wanatesa life kiasi kile basi hata mm naanza kuelewa na kupata mwanga kwa nn always nilionekana mnyonge kwa kuhisi sina bahati ya mkono wa pesa. Nina kazi nzuri, mshahara gross karibu 3m lakini wapi bana nasomesha vitoto viwili englsh medium na mke wangu tuna gari moja tu lakini hata nyumba sijamaliza. nikawa najiuliza labda sijui badget nn? watu wanatesa daily viwanja, shopping mpaka za mbwa wao, majumba magari, mavazi, cm jamani tz hii hii? tena wanaamka muda wanaotaka, ukiuliza itasikia, msanii huyu au anaduka la nguo au mwanamichezo au urembo tu nk. Nikajiuliza hawa wanamuomba Mungu huyu huyu ninamjua au wenzangu wanaonana nae kabisa na kumshika mkono?kama ni Mungu huyu mbona mm sitokei? Anway nimepata jibu tu coz hata mm ningepata fursa hio ningeitumia for sure ila naona nimechelewa, kwa waliowahi hongera zao na kama hujakamatwa jipange vzr cc tupo tunawasubiri kitaa.

    ReplyDelete
  3. list ya wasanii,watoto wa mjini wa uza unga ni kubwa mno mpaka wacheza mpira watangazaji ni mapunda

    ReplyDelete
  4. Hii ni hatari,taifa linaangamia,jaman tuoneane huruma na turidhike na tulichonacho hakika tamaa mbaya!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad