Waziri Mkuu Bw.Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam , itupilie mbali kesi iliyofunguliwa dhidi yao na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kuwa kituo hicho hakina haki kuwafungulia kesi hiyo.
Hoja za Msingi walizozitoa za kuomba kesi hiyo ifutwe ni:
1. Kesi hiyo haipo kisheria na Sheria ya Kinga , Haki na Madaraka ya Bunge;
2. Kesi hiyo inapingana na sheria namba 6 , Kanuni ya 3 ya kesi ya madai pamoja na amri ya 28 na kanuni ya kwanza ya sheria hiyo;
3. walalamikaji katika kesi hiyo hawana haki ya kufungua shauri hilo, kuingilia shughuli za Bunge ambapo amri zinazoombwa na mdai(LHRC), haziwezi kutolewa kwa sababu zinaenda kinyume na sheria za msingi.
Mahakama imetoa siku 14 kwa LHRC kuwasilisha majibu ya hoja za pingamizi hilo la awali ambalo limewasilishwa na AG pamoja na BW. PINDA.
Jana nimeota Rais ajaye atakuwa Mizengo Pinda, afu ndoto zangu siku zote zinakuwa kweli
ReplyDeleteushindwe na ulegee tena ondoa minuksi ya ndoto zako peleka kwenu
ReplyDelete