Habari iliyokuwa inasambaa ni kuwa mwanamke huyo aliyedhaniwa kuwa ‘white widow’ alitoroka kwa njia ya kujifanya kumsaidia mwanamke huyo (kwenye picha hapo juu).
NTV ya Kenya iliamua kusahihisha habari hiyo kwa kumtafuta mwanamke huyo (kushoto katika picha) na walifanikiwa kumpata na kuweka taarifa hiyo sawa kwa kukanusha kutokuwa mtu ambaye watu walimdhania.
Akiongea na NTV Mwanamke huyo alijitambulisha kwa jina la Henna, na wakati wa tukio alikuwa katika mall ya West gate na wanae wawili pamoja na dereva wakifanya manunuzi ndipo ghafla mashambulizi yakaanza. Wakati wa kujiokoa aliamua kuwa msamaria mwema kwa kumsaidia mwathirika mwenzie aliyejeruhiwa kama ilivyoonekana katika picha iliyozuwa uvumi wa kuwa ‘white widow’.
Mtazame hapa