Katibu wa Itikadi na Uendezi wa Chama Cha mapinduzi (CCM),Nape Nnauye amemtaka Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe kujiuzulu nafasi hiyo mara moja kwa sababu ameshindwa kuiongoza kambi hiyo.
Wito huo uliutoa mjini Shinyanga Ijumaa jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana katika mkoa huo.
Nape alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni Bungeni ni uthibitisho wa wazi kuwa,Mbowe ameshindwa kuiongoza kambi hiyo kwa kuwa kabla yake hakukuwahi kuonekana fujo na vurugu kama hizo katika chombo hicho kinachoheshimika.
Alisema udhaifu wa Mbowe katika kuiongoza kambi hiyo ndiyo unaosababisha ishindwe kufanya kile ambacho Watanzania wanakitarajia kutoka kwa wapinzani.
Alisema wanasiasa ambao wanasababisha na kushabikia fujo na vurugu hawafai kwa madai kuwa wanaipeleka nchi mahali pabaya.
Hata hivyo, alisema hilo halitafanikiwa kwa sababu Serikali, CCM na Watanzania wapo makini dhidi ya mtu yeyote anayepanga kuwachonganisha. Aliishangaa Chadema kwa kushinikiza wabunge waongezwe kwenye Bunge la Katiba huku ikitaka wengi wa hao watokane na wanasiasa.
“Chadema inataka wawakilishi wa wakulima wawe kumi tu wakati wakulima ni asilimia 80 ya Watanzania wote. Hivi kweli wana lengo la kuwatetea Watanzania au maslahi binafsi tu,?”alihoji Nape.
Nape waliwataka wananchi kufanya uamuzi wa busara wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu .
Naaapeee!!! Umechemka na kauli zako za kitoto eti .MBOWE ajiuzulu kwa lipi ??? Unakumbuka sakata la JAIRO kunuka rushwa tena akilihusisha BUNGE na serikali yenu chakavu ya CCM mkapaka manukati uozo huo sasa mbowe kipi ambacho kafanya wakat naibu spika analeta ushabik mjengoni. NAPE uwe unaangalia vya koropoka ucwe ka MCHEMBA anae miliki ka degree kamoja na kusema ye msomi anaefaa kiliongoza taifa
ReplyDeleteAza wewe kwanza na chama chako kibovu, MBOWE jeshi wewe unafikili kama ww mtoto wa mama, we c kibalaka wa ccm, Puumbaafuuu!!
ReplyDeleteMnafiki mkubwa wewe
ReplyDeleteNape umechenka tena komaaa
DeleteNape huna lolote...maviiiiii
DeleteNAPE na wewe unatafuta kiki kupitia kwa MBOWE Puumbaafuuu!!!
ReplyDeleteHivi wewe nape utoto utauachalini. mmekuja shy na kinana wako mkakosa watu viongozi wa ccm shy wakakusanya. watu wenu kwenye mafuso hatahivyo hamkupata watu sasa unakuja na mbowe. ajihuzu mwambie wazori wenu wa nishati ajiuzuru kwani kawa tuka watz kwamba gesi waachane nayo wa tengeneze jusi.m ng.machimkenda
ReplyDelete