NAPE AMWITA MBATIA MNAFIKI KWA KUWAUNGA CHADEMA MKONO SAKATA LA KATIBA

Siku chache baada ya Mwenyekiti  wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James  Mbatia kuungana na Chadema pamoja na CUF kupinga kusainiwa kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuendesha maandamano nchi nzima, Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye amekiita kitendo hicho kuwa cha kinafiki.

Nape alisema kitendo cha mbunge huyo kuungana na vyama vingine kupinga suala hilo  ni kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete aliyemteua kuwa mbunge kwa kumwamini kuwa mchapakazi, huku akiongeza kuwa kitendo hicho ni unafiki mkubwa.

Nape aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana kukagua utekelezaji  wa ilani ya CCM.

Alisema Mbatia aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa mbunge kutokana na kuonekana kuwa mchapakazi, huku akiongeza kuwa  kitendo alichokionyesha  mbunge huyo ni kumgeuka Rais kama kinyonga

Nape alienda mbali zaidi na kuongeza kuwa hatua ya mbunge huyo kuungana na wapinzani  siyo sahihi na haikubaliki hata kidogo, huku akimtaka kujiuzulu nafasi aliyopewa kwa heshima  na Rais,.

Katibu huyo mwenezi aliongeza kuwa viongozi wa Chadema wakiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Dk Willbrod Slaa pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lisu, wamekuwa wakitumia matatizo ya Watanzania kama mtaji wao wa kisiasa na kwamba viongozi hao hawana aibu.
-Mwananchi
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nape...wewe tunakufaham vzr ni mnafiki mkubwa..mbatia anasimamia maslahi ya watanzania na si ya Ccm

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amaaaa kweli..nape unataka. kusema wote wanaoteuliwa na jk wasimamie upande wa ccm?

      Delete
  2. Nape mbumbumbu tu analoweze ni makelele tu

    ReplyDelete
  3. Hivi nape utoto utaachalini.unaonaulivyo zuzu inamaana. hujui kazi za mbunge.kazi za mbunge ni kuisimamia na kuishauri serekali hajalishi anechaguliwa kwa kura au kateuli.jk wakati anamteu mbatia alujua hayo. wewe unafikiri na sawa nawewe nawezio jk aliwapa nafasi kishikaji bwege ww.m.ng.machimkenda

    ReplyDelete
  4. Kwanini J.K asimteme huyo nape. Maana anafanya "msielegeeeeeeeeeeeeeeeeee"

    ReplyDelete
  5. Ivi uyu Nape ana elimu gan?..

    ReplyDelete
  6. Izo mada nyingin we nepi ue unakaaa mabarazan na kina mama ndo mnaongea co unaongea mbel za wa2

    ReplyDelete
  7. Kweli Nape una akili ya rangi ya kijani, na sidhani kama itakupeleka mbali unasukutulia maji yake nini. Acha umbelembele. tendeni haki,.

    ReplyDelete
  8. Kweli Nape una akili ya rangi ya kijani, na sidhani kama itakupeleka mbali unasukutulia maji yake nini. Acha umbelembele. tendeni haki,.

    ReplyDelete
  9. Kweli Nape una akili ya rangi ya kijani, na sidhani kama itakupeleka mbali unasukutulia maji yake nini. Acha umbelembele. tendeni haki,.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad