NIMEVUNJA UCHUMBA WA MFANYAKAZI MWENZANGU KUMUOKOA RAFIKI YANGU..SIJUTII

Ndugu zanguni akina dada,kaka akina baba na akina mama na wote mlio kwenye ndoa maandiko yanasema ndoa na iheshimiwe na watu wote tena wote, in short nimemuumiza dada mfanyakazi mwenzangu lakini sijutii hata kidogo.Ni kwamba dada ameanza kazi kama mwaka mmoja uliopita akatukuta sisi wakongwe tumetulizana ndani ya ofisi.Kutwa huyo dada ni kumzoea kila mwanaume ndani ya kampuni nzima anajifanya eti social wewe chezea Dar.

Baisi bi dada watu wakaanza kumfukuzia na wenye visu vikali wakala nyama, mimi nikamwendea nikamwelezea kuwa anatakiwa ajitahidi kuwa mtulivu maana vijana wote mle ofisini tuna commitment zetu kwenye either ndoa ama mahusiano na wengine inasemekana wameathirika.Mimi akaniona eti mshamba natokea huko kwenye mkoa wa Operation Kimbunga.Sasa juzi kati kuna jamaa yupo njema ile mbaya akaniambia kuwa amepata mchumba na mchumba mwenyewe tupo kampuni moja kwa hiyo akawa ananiomba ushauri, nilivomuuliza akanitajia jina la bidada ambae kila siku nilikuwa namuambia atulizane.Yaani sikupepesa macho niliamuambia kila kitu kinachohusiana na huyo dada bila kuficha hata nukta.Jamaa kabwaga manayanga na wala sijutii moyoni ni sawa kabisa.Bottom line kwa wanaweke na wanaume tulizaneni na ndo zenu na kwa wakaka na wadada kama mnategemea kupata wenza waliotulia basi na nyi tulieni.

Source:JF
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huna hata haya we mwanamke una liroho libaya had linanuka,huna lolote wivu tu unadhan hatuwajui nyie wanawake?

    ReplyDelete
  2. Na kweli roho mbayaaa inanuka kabisa shenz na kweli umetoka ng'ong'ona au ulikua unataka akuoe auu? N ther z no a perfect human bng bichwa wewe

    ReplyDelete
  3. Sawa sawa dada umefanya vizuri sn na ndo wengne wajifunze! Hamna cha roho mbya! Alitaka ampelekee mwenzie vilivooza! Huko huko na umalaya wke...

    ReplyDelete
  4. Ukickia ushakunaku ndo huooo,inaonyesha ulikuwa unamtaman sana huyo jamaa,sasa kwa tarfa yako mshikaj atatafta mwingine haji kwako ng'oo

    ReplyDelete
  5. Asa we ulipata faida bhana hapa mjini kila mtu na maisha yake we paka mdogomdogo nini?

    ReplyDelete
  6. huna jipya huna la kufanya nazani hujui kuwa kila shetani na mbuyu wake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad