Kwa mujibu wa taarifa za sasa, takriban watu 20 wameripotiwa kuuawa na wengine 50 kujeruhiwa wakati ambapo mapambano ya bunduki yanaendelea kati ya polisi na watu hao wenye silaha walioiteka mall ya Westgate jijini Nairobi, Kenya.
Shuhuda mmoja anadai aliwasikia watu hao wakiwaambia waislam wasimame na kuondokoa na kwamba wasio waislamu pekee ndio waliwalenga.
Askari wa ulinzi walionekana wakitoa miili iliyotapakaa damu ikiwa imeweka kwenye matoroli ya supermarket.
Huduma ya kwanza ikitolewa kwa majeruhi
Balozi wa Uholanzi nchini humo Rob Vandijk ameliambia shirika la AP kuwa alikuwa akipata chakula kwenye mgahawa uliomo ndani ya mall hiyo pindi watu hao wenye silaha waliporusha bomu hilo. Polisi wameizingira mall hiyo na harakati za kuwakomboa watu walioshikiliwa mateka kwenye mall hiyo zinaendelea.
Ndugu wa baadhi ya watu walio ndani ya mall hiyo wakiwa na majonzi
Mall hiyo ni maarufu kwa kuwa na wateja wengi wenye kipato cha juu nchini humo na raia wa kigeni. Polisi imewataka wananchi wakae mbali na eneo hilo kwakuwa bado ni hatari.
Sababu za shambulio hilo hazijafahamika lakini vyombo vya habari nchini humo vinasema kundi hilo laweza kuwa magaidi ama majambazi walioenda kupora.
Polen wakenya kwa mkasa huo.
ReplyDeleteAl-shabaab.
ReplyDeleteJaman inatishaaa na kuckitisha polen sana
ReplyDeletePoleni wakenya hilo ni janga lakitaifa
ReplyDeletePoleni ndugu zetu wakenya
ReplyDeleteSo sad.poleni wapendwa..
ReplyDeletePole saana wenzetu
ReplyDeletePole saana wenzetu
ReplyDeleteJaman tujifunze Wa tz, je ulinzi Wa MLIMANI CITY UNARIDHISHA?? yasije kutokea tena haya
ReplyDeletekalinde wewe. unawajua al shabab au unawasikia.
DeletePoleni sana ndugu zetu wakenya,
ReplyDeleteIT WAS SAD DAY IN KENYA HISORY
ReplyDelete