MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.
Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo
“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka.“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C.
Source:Global Publishers
Ray C ajui nini manaana ya kuokoka.........Kuokoka ni kuamini na kuacha kutenda maovu
ReplyDeletehao walokole wenyewe ndo wanaongoza kwa kila maovu na wenyewe mashuhuda. hongera ray c kwa kutokua mnafiki kama wafanyavyo wengine.
Deleteby MR EVIDENCE
UCPENDE KUWEKA WAZI MAMBO AMBAYO WA2 WENG HAWANA FAIDA NAYO, KAMA SUALA LA KUPIMA VVU/UKIMWI, HII N PRIVATE ISSUE. NAN KAKWAMBIA UNA UKIMWI?? NA KAMA ULIKUWA UVUMI...SAA NYINGNE UCWE NA PRESSURE NA UVUMI WA WA2 AMBAO UNAJUA NI TOFAUT NA MAKUSUDIO YAKO "MTI WENYE MA2NDA HAUKOSI KUPIGWA MAWE" MAKE WANATAKA WATOE HAYO MA2NDA, CHUKULIA POA ISSUE KA HZO.
ReplyDeleteCHA MSING MSHUKRU MUNGU MAKE KAKUTOA SEHEMU HATARI AMBAYO HAIKUWA EASY KUTOKA BILA YEYE.....ASANTE GO KWA HLO....AMEN!
NA KINGNE, WE NI MSANII AMBAYE KLA M2 ANAHTAJI KAZI ZAKO, KO HUNA BUDI KURUDI MAPEMA KWENYE GAME....BADO 2NAKUHTAJI KWA VYOVYOTE VILE.
ACHA MAMBO AMBAYO KUNDI LA WA2 WENG HAWALIPEND JAPO HATA WE UNALPENDA, UTAKUWA UMEVUNJA MWENENDO WA MAISHA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA, WENG WANAIGA KWAKO....
Hapo Rac C ulikuwa na rangi nzuuuri, sasa hivi kiruuu umejipigaje deki? Hayo ni maamuzi yako binafsinya kiimani bora tu unamwamini Yesu na Mungu baaaasi!! Mungu atazidi kukubariki maana neno lake ni uzima tosha. Luv u Rehema
ReplyDeleteWatu wanapenda kumbeep Mungu! Kuokoka ni siku yakufa kwako basiii..wewe mwanaadam sio mtume hujasafishwa kwa hiyo zambi utazitenda tu..kikubwa nikufanya ibada mengine tumuachie Mungu mwenyewe. Eti watu huwa wanaokoka, okoka my ass! Sisi nibinadam kukosea ikawaida ndio tulivyo ubwa kikubwa ni kusali kwa kumshukuru Mungu na kumuomba mwisho mwema! I love u Ray to the C
ReplyDelete