RWANDA YAPANDISHA USHURU WA MAGARI YA MIZIGO YANAYOTOKA TANZANIA

Serikali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara (ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo (Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi, kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka Rusumo  ambapo  ni  mpakani mwa Tanzania na Rwanda na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo yana plate number  za Tanzania.

Wamiliki wa Malori wameiomba serikali kuingilia kati ili kunusuru hali  hiyo.

 Credit:JF

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo la Kagame ni elimu ndogo, form II mtu anaendesha nchi?Kauli aliyotoa Kikwete ilikuwa nzuri sana.Kagame amekasirika kwa Tanzania kupeleka majeshi Congo, na kwa upeo wake mdogo ndipo anaudhihirishia ulimwengu kuwa ana wasaidia waasi wa M23. Niko chuo kimoja nje sitataja wapi maana najua kagame anawafuatilia sana, kuna dada mmoja mnyarwanda aliniambia mwaka jana.. mara nyingi amekuwa akimpigia kaka yake mwanajeshi wa Rwanda ana mwambia wako Congo wana fight, report za UN zimeonesha hivyo.Huyu jamaa na Clinton wameiharibu Congo(nchi yenye utajiri mkubwa duniani lakin ndio masikini namba moja) . Leo hii kila baada ya miezi 2 Clinton lazima aende Rwanda, kuna nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Clinton huwa anaona aibu sana kuwa wakati wa mauaji ya Rwanda yeye akiwa Rais wa Marekani hakufanya lolote kuyazuia. Kutokana na aibu hiyo amejitahidi kujisafisha kwa kujifanaya anaisadia na kuitetea sana Rwanda hii ya Kagame akiwa nje ya madaraka.

      Delete
  2. Ndio maana juzi Clinton alimsifia Kagame, akisema hizo ni shutuma tu hazijadhihirika mbele ya mahakama.Congo ilitakiwa kuwa na uchumi mzuri kuliko hata nchi za ulaya, maana asilimia 75 ya madini yanayotengeneza simu, laptop na bdhaa nyingine yanatoka Congo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad