STAA WA BIG BROTHER MWISHO MWAPAMBA AELEZEA JINSI ANAVYO BAGULIWA NAMIBIA

STAA wa Shindano la Big Brother, Mwisho Mwampamba, amesikitishwa na vitendo vya ubaguzi alivyofanyiwa na Polisi wa nchini Namibia, anakoishi na mkewe, Meryl Shikwambane, ambapo walimfuata kwenye nyumba yake na kumtaka aondoke nchini humo.

Mwisho ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akisema nchi hiyo sasa hivi imekuwa kama Afrika Kusini, ambako wageni, hasa wenye ngozi ya Kiafrika, hupata shida ya kuishi kutokana na kubaguliwa.

“Mimi nimeoa mtu wao na nimezaa naye mtoto, nashangaa kubaguliwa na polisi hao, pia inashangaza kuona wakiwahudumia vyema wageni kutoka barani Ulaya, lakini sisi Waafrika wenzao tunabaguliwa,” alisema Mwampamba.

Mkali huyo ameshangazwa kupewa hati ya kuishi nchini humo kwa miezi miwili pekee, wakati ameoa mwanamke wa nchi hiyo, huku akipata shida hiyo hata mipakani.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Polisi wa kiafrica ndivyo walivyo hata majuzi tu kuna wahamiaji haramu wameolewa na watz kwa zaidi ya miaka 20 wanaambiwa waondoke

    ReplyDelete
  2. ukoloni mamboleo, viongozi vibaraka nk. ndio sababu ya matatizo hayo na ogopeni sana vyama vya siasa vinavyowezeshwa kifedha sana na nchi za kimagharibi kwani baadaye watahitaji manufaa kutoka kwenu.
    "ukila lazima nawe uliwe".

    ReplyDelete
  3. we mwanzo cjui mwisho c urudi kwenu morogoro? unabaguliwa na bado unang'ang'ania utadhani umeua kwenu? au mpk operation kimbunga ikukute na wewe huko?

    ReplyDelete
  4. Hiyo ndio hali halisi ilivyo, ni wakati sasa Watanzania mtambue kwamba nchi zote za Afrika na hata za Ulaya zinatuthamini tu pale zinapokuwa na maslahi na sisi, ni kwamba tu watu wengi walioko nje ya nchi huwa hawataki kusema tu ni manyanyaso kiasi gani huwa wanakutana nayo, sehemu pekee katika dunia hii ambayo mtu mgeni aliweza kuheshimiwa na kutukuzwa kuliko mwenyeji ni Tanzania, baadhi ya nchi za kiafrika ziliweza kuwaheshimu raia wa Tanzania kipindi kile tunazisaidia wakati wa harakati za ukombozi na mara baada ya harakati hizo kuzaa matunda na kuweza kujikomboa, kwa sasa zinafanya juhudi kubwa kuweza kuwainua watu wao na baada ya muda mfupi Watanzania waishio nchi hizo watafukuzwa warudi kwao, kwahiyo ilichobaki ni suala la sisi kutengeneza mazingira mazuri ya kuishi hapa nyumbani Tanzania na kipaumbele kikubwa wapewe Watanzania wenyewe, hii itatusaidia tusionekane wajinga wa kupindukia kwenye jumuiya ya kimataifa.

    ReplyDelete
  5. Siurudi nyumbani wew unang'ang'ania nin uko,cku nyengine uc2sumbue sis

    ReplyDelete
  6. serikali ijifunze kuweka mazingira mazuri ya watanzania kwani itafikia wakati kila mtu kwao sasa na wewe huko umeolewa au umeoa utaoaje alafu ukae ukwenu nilazima utanyanyasika rudi na mkeo nyumbani kwenu ili mjipange kimaisha tanzania bado nafasi ziko nyingi alafu unangangania huko

    ReplyDelete
  7. pole bulaza wangu wa moro,achana na hao makuma,wanapapatikia ngozi nyeupe tu,mungu yu nawe

    ReplyDelete
  8. RUDI KWENYU NDILO ULILOTAKA HILO UNAFIKIRI WAO NI KAMA NYIE KILA KONA MMEJAZA WAGENI NDIO MJIFUNZE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad