SUGU "NDUNGAI ALIAMURU ASKARI WANIPIGE BUNGENI"

NI kauli iliyotolewa na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema tukio la kupigwa ngumi na askari ndani ya Ukumbi wa Bunge lilisababishwa na  amri ya Naibu Spika, Job Ndugai na wala siyo askari.
Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai  askari.
‘Sugu’ alitoa kauli hiyo  wakati akiwahutubia wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo ziarani  mkoani Mbeya  wakifanya  mikutano na wananchi kwa lengo la kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na  wabunge wengine bungeni hivi karibuni.
‘ Sugu’ alidai kuwa Ndugai ni adui wa wapinzani bungeni na kwamba kwa vyovyote vile ilikuwa vigumu kuvumilia kwa mtu yeyote baada ya askari kuanza kupiga wabunge kutokana na amri ya  Ndugai.
Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema kitendo alichofanyiwa Sugu hakikuwa kibaya kwake peke yake, bali hata wananchi waliomchagua.
Hata hivyo, Dk Slaa  alisema kwa upande mwingine ili heshima ya Bunge lolote lile duniani  iwepo, ni lazima wabunge watandikane makonde ndani ya Bunge  na si vinginevyo hivyo hashangai kwa kilichotokea kwa Sugu bungeni.
Dk Slaa, alimjia juu Ndugai akisema alikiuka Kanuni za Bunge kwa kitendo hicho na  kubainisha kwamba kanuni za Bunge zipo wazi kabisa  kwamba iwapo itatokea vurugu ndani ya Bunge anachotakiwa kukifanya ni kuahirisha Bunge kwa wakati huo.
Pia alisema askari ambao ni  wapambe wa Bunge ‘Sargent at arms’ ndio wenye mamlaka ya kuingia ukumbini na endapo itatokea nguvu ya ziada hao ndio wanaotakiwa kisheria na siyo kuwaita askari wa nje ya Bunge kuingia ndani.
Dk Slaa alisema kitendo kilichofanywa na Sugu pamoja na wabunge wengine ni cha kijasiri na aliwataka kutokurudi nyuma na misimamo yao  bali waendelee kusonga mbele.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jaribuni kuongea kiswahili fasaha kwenye R mnaweka L kwenye L mnaweka R eti fikilieni (fikirieni)kufikilia (kufikiria)

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad