TAARIFA INAYOSEMA HUENDA MAGAIDI WA WESTGATE WALITOROKEA NJIA YA MAJI TAKA CHINI YA JENGO HII HAPA

Wakati bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya, mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.

Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.

Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.


Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.

Chanzo kimoja kilisema “They escaped like sewer rats. The terrorists would have been able to pass through the underground tunnels at a rapid pace and surface almost unnoticed”.


Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.

Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi

-BONGO5

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chezea Al-shabab wew walijipanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAO NI NDIO WANAUME, UNADHANI MARA NYINGINE WATAPIGA KWENYE MA-MALL TENA, KWANI WAO WAJINGA.

      Delete
  2. Mmmm hawa watu kiboko...!

    ReplyDelete
  3. Tusiseme ati hawana akili ama wajinga mm nadhani ingetumika njia ya kutafuta suluhu mbona nchini Congo kuna suluhu,n.k sasa huku kuna nn?na wao wanajisikia uchungu watoto kuuawa wanwake kubakwa n.k,unajua sisi bado tunafuata mitizamo ya Marekani kila kauli atakayotoa marekan sisi kwetu ndy mzee,jaman hata ukiwa na rafiki mwenye uwezo ukiwa kwake kila kitu mzee mwishowe atakuona bwege na hatimaye atakuchulia mzigo(mke) tuache propaganda za Marekani na washirika wake wawo wanamaslahi,

    ReplyDelete
  4. Hizi habari kila cku zinatoka mpya,tuamini ipi!acheni redio mbao kuwapotosha watu,imekuwa desturi mtu anakaa na kutunga habari na kuposti mtandaoni.

    ReplyDelete
  5. alshabb n wanyama c watu kabisaa...

    ReplyDelete
  6. Mdau 5:43 hapo juu umeongea kweli kabisa

    ReplyDelete
  7. Daa! Waafrika tunauwa kinyama hivi jaman kwa ya fitina za hawa wasenge wazungu hebu tubadirike jamaa tuijenge africa yetu tuache kujipendekeza kwao mbona wenzetu wachina wameweza. Hawa jamaa wameona afrika iko na utajiri mkubwa sana kwa hiyo uli wapate kuvuna mali zetu wanatumia njia ya kutugombanisha.

    ReplyDelete
  8. al shabashaba hawataki kuchezewa na nchi yao kwanza hawapendi shobo.

    ReplyDelete
  9. Sio tunauwa bali tunauwana inaonesha una hasira sana ndugu pole sana.

    ReplyDelete
  10. nafikiri sasa majengo yote yasiwe na bomba kubwa za maji taka maana ho watu nahisi hawajamaliza kazi zao maana hata kuna muv fulani fulan ulaya or marekan zimewai onyesha watu wanatorokea kwenye bomba za maji machafu hii sasa ni live naona tubadili mifumo ya ujenzi ili wabanwe mi naona kwa kweli kazi ilikuwa ngumu thats why hawakuwaza hizo njia i present....

    ReplyDelete
  11. sasa kama haapatakuwa na mabomba ya maji taka hayo maji yatakwenda wapi cha msingi waongeze tekniki za ulizi maaana walijisahau wao wanajua kuna mabomba yanayoweza kupitisha mtu kwanini hizo sehemu zisilindwe hilo nifundisho kwa wote sio wakenya tu

    ReplyDelete
  12. Jiulize kikwete kajipanga na m23?
    Sio unakaa kusimulia ya Wakenya akati na Tanzania pia inaleta mambo ya uchokozi kwa kupeleka majeshi huko kongo mi nawashangaa sana watu mnaona raha tu mnafikiri m23 ni kama nduli dada hawa wanasaidiw na nchi karibu 50

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad