Wapenzi wa mmu, naomba nipewe pole kabla sijaanza kusimulia mkasa ulionipata jana alhamis ya tarehe 12 mwezi wa 9. Siku hiyo niliyoitaja hapo, ndoa yangu ya miaka 10 iliingia katika msukosuko mmoja mkubwa sana.
Kama kawaida yangu nimetoka kibaruani mnamo saa 12 jioni. Kufika nyumbani tofauti na siku nyingine, nabisha hodi mai waifu wangu yuko kimya sebuleni. Nikamsalimia kama kawaida yangu "darling hujambo"? Nilishangaa mke wangu kulipuka kama bomu la mbagala na kuniambia "ukome kuniita hivyo, kamuite mama Siwema". Kabla hata sijapata tafakari ya kilichokuwa kinaendelea nikarushiwa karatasi ambayo ilikuwa na maneno yafuatayo:- Mpz baba Siwema, tangu umetoka safari hutaki kuja kutuona umeng'ang'ania kwa huyo kinyago cha mpapule wako unadhani sisi tunaishije? Kama ulijua kwamba hutaweza kutunza mtoto kwa nini ulinipa mimba? Nimemtuma Siwema umpe pesa za matumizi aniletee, ikishindikana nitakuja mwenyewe tuonane mbele ya huo unayemwita mkeo.
Nikamuuliza mke wangu hii barua imetoka wapi? Jibu ni kwamba imetoka kwa mke wako ambaye hata hutaki nijue ulishazaa naye mtoto. Akaendelea; amekuja hapa motto na barua hii anakutafuta wewe, nikamuulize kama anakufahamu akasema ndiyo na kila mara mama yake huwa anamtuma kwako unampa pesa anampelekea.
Kwa kweli hizi taarifa zilinichanganya sana maana mwanamke mwenyewe hata simjui ila ni kweli nilikuwa safarini mwanza na nimerudi jumapili iliyopita. Mke wangu aliendelea kufura kama mbogo hadi nikaiona sebule imekuwa ndogo.
Wakati nikiendelea kutafakari hatima ya ndoa yangu mtoto wa kike akapiga hodi, kuingia tu mke wangu akesema "mtoto wako mwenyewe huyu hapa, sasa mpe pesa ampelekee mama yake". Kale kakasema, hapana baba yangu siyo huyu. Baba yangu jina jingine anaitwa baba Eric. He! ndiyo kutambua kwamba yule mtoto alikosea nyumba ya baba Eric akaingia kwangu.
Mke wangu aliniomba msamaha na kesi ikawa imeishia hapo. Lakini nilionja joto ya jiwe.
From Jamii Forums
Akuna pole hapa,
ReplyDeleteDuh...big pole kwa kweli.....!!!
ReplyDeletePolesana!
ReplyDeletekwenda.
ReplyDeletekwenda.
ReplyDeletePole ndugu huwa inatokea mambo kama hayo, pole sana!
ReplyDeleteYote maisha mkeo anakupenda sana ndo mana anakuwa mkali akiona anataka kuibiwa, wenyewe wanauita WIVU usiache mke huyo ww anakufaa sanaaaa!!
ReplyDeleteYote maisha mkeo anakupenda sana ndo mana anakuwa mkali akiona anataka kuibiwa, wenyewe wanauita WIVU usiache mke huyo ww anakufaa sanaaaa!!
ReplyDelete