WALTER CHILAMBO "NAY WA MITEGO FANYA UCHUNGUZI KABLA YA KUONGEA"


Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012, Walter Chilambo ana ushauri kwa Nay wa Mitego. Afanye uchunguzi na utafiti wa kina kabla ya kuongea mambo kwenye nyimbo zake.

Bongo5 ilikaa na staa huyo wiki iliyopita kuzungumzia wimbo wa Nay wa Mitego, Salam Zao ambapo alisema Walter amepigika licha ya kuwa mshindi wa milioni 50 mwaka jana.

“Kwangu kidogo alikuwa wrong kwasababu mimi sipo hivyo yeye anavyozungumza, inabidi angefanya uchunguzi kwanza kwamba sina hata baiskeli au naishi vibaya au siwezi kula, siko poa, angefanya uchunguzi kwanza halafu ndio angeongea,” alisema Walter.

“Lakini mimi simlaumu, kaongea ambacho yeye anakifeel.”

Katika hatua nyingine, Walter amesema yupo mbioni kufanya video ya wimbo wake wa sasa, Doro.

Source:Bongo5
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad