UWEZI AMINI TANZANIA IMETEGWA TENA KATIKA MKUTANO WA EAC

NCHI za Tanzania na Burundi, kwa mara nyingine zimetengwa na wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana mjini Kigali jana. Marais hao walitarajia kujadili namna ya kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia uimarishwaji wa miundombinu, uchumi, biashara pamoja na kuweka mikakati ya shirikisho la kisiasa.

Kitendo cha kuziacha Tanzania na Burundi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kinazidi kutia shaka mtangamano wa jumuiya hiyo.

Nchi hizo mbili zimeshaeleza kusikitishwa na muungano wa nchi hizo tatu, ambao zimesema unakwenda kinyume cha makubaliano na mkataba wa EAC.

Katika mkutano huo, marais hao, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, pamoja na mambo mengine, walitarajia kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya ushuru kinachotarajia kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kutoka Mombasa nchini Kenya, Uganda hadi Rwanda.

Aidha Sudan Kusini ilialikwa ikiidhinishwa kama mshirika katika kikao hicho.

Mkutano huo unakuja baada ya ule uliofanyika mjini Kampala, Uganda, Juni mwaka huu na mwingine uliofanyika Mombasa, Agosti, ambako viongozi hao watatu walipendekeza kupanuliwa kwa Bandari ya Mombasa, ili kuwezesha uharaka wa bidhaa kupitishwa katika kuhudumia kanda nzima.

Mkutano mwingine wa marais wa nchi 15 za Afrika, ikiwamo Tanzania, utafanyika leo nchini hapa, katika kongamano la siku nne ambalo linatarajiwa kuweka kipaumbele kwa uimarishwaji wa huduma za internet katika mataifa hayo.

Kwa mujibu ya waandaaji, zaidi ya wajumbe 1,500 watahudhuria mkutano huo, chini ya uenyeji wa Rais Paul Kagame na Dk. Hamadoun I. Toure, Katibu Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Kiteknolojia (ITU).
-Mtanzania
Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WAACHENI WATUTENGE HAO WOTE WANATAWALA KWA MKONO WACHUMA KIKABILA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tanzania is a great country that can go far without kenya, uganda and Rwanda. the only move going on here is a competitive economic war between Tanzania and kenya, uganda and rwanda are just used by kenya without their knowledge. for a land locked countries like uganda and rwanda to put their feet on one side its dangerous because when things go bad in kenya you will have no place as altenative. you ignore and subortage Dar port, there are times when you will need dar port and Tanzania will raise fees for you because you will not be friend with him. as a wise president/country uganda/rwanda you will be in a better position to have two altenatives both kenya/mombasa and Tanzania dar port. because there are times you never know you will beg tz. no one knows what the future holds for you. uhuru kenyatta is using you as an instrument to retaliate Bagamoyo port and the massive development in tz, unfortunately the chinese have put both feet into tz and there are many wonders not yet disclosed which will make kenya speechless. think about this uganda.

      as for rwanda, tz does not even want to waste time thing about them, because they add very little to tz. i only pray kagame opponents or even museven won't be trained by tz to overthrow the dictatorship if tz turns enemy of these two dictators. if i were president of tz, i would be training kayumba nyamwasa and others today to bring down kagame. but for tz, the only punishment for rwanda is to block the m23 and goma/kivu etc where minerals are smuggled from congo to build rwanda, there the only place rwanda/kagame gets pride of money, other wise, they will depend on selling coffee, tea and women.

      Delete
  2. Kikwete. Atabaki Na. Bandari yake sababu Ya ushuru usiokua Na kichwa Wala miguu ngoja wahamie bandari Ya Mombasa Ndio tukomee

  3. Jamani hamjamsikia waziri Membe akifafanua hilo? Tatuwezi kukubariana na natakwa yao waacheni waandelee, na wewe kama huna cha kuandika kwani lazima uandike?

    ReplyDelete
  4. hii yote imetokana na kuwakubali hao warwanda na burundi kuingia africa mashariki ...mbona mwanzo tulikuwa atuko hvyo tulivyokuwa nchi tatu hayo manyarwanda yamekaa kwenye vita sasa yameingia yanachonganisha watu fu....ck..kagame

    ReplyDelete
  5. UNAJUA MSIMLAUM JK KWANZA ANAJITAIDI NINGEKUA MIMI NIMESHAKIMBIA RASHID NKYA

    ReplyDelete
  6. TUTENGENI KWENYE SHILIKISHOLENU LAKINI MUJUWE MUKIPIGANA TENA VITA HAKIKISHENI MUNAPO PAKUWAWEKA WAKIMBIZI WENU ALAFU WEWE MUSEVENI NINI KUJIPENDEKEZA KWA HAO WAKABILA WATU WENYE HULKA ZA KUBAGUANA UNATAKA KUSEMA UMESAHAU KWAMBA HAPO ULIPO NIKWAJUHUDI ZA NYERERE LEO HII UNASHIKIWA AKILI NAWATOTO HAO KISIYASA ACHA KUJITOWA FAHAMU AKILI YA KUSHIKIWA CHANGANYA NA YA KWAKO

    ReplyDelete
  7. WANACHO FANYA HAO VIONGOZI NI SIYASA NA SIYO MATAKWA YA WANANCHI WAO WANANCHI WOTE WA EAC WANA USHILIKIYANO MKUBWA KULIKO WAKWAO WA KISIYASA WENYEWE WANA FANYA BIASHARA WAKATI MWENGINE KWA SILI ILI WANASIYASA WASIJUWE KAMA HAMUWAMINI NGOJENI BANDALI YA BAGAMOYO IJENGWE WATAONA AIBU WAO WATAFANYASIYASA ZAKUBAGUWA INCHI LAKINI WANANCHI WATAKUWA WAMOJA INCHI ZOTE

    ReplyDelete
  8. safi sana Tanzania siasa nyingi na kufuatialia maisha ya watu,waache waungane walisongeshe sisi tubaki kutoka mapovu kwenye blog.

    ReplyDelete
  9. waache waende na vichwa vya train watakapo kumbuka kuwa mabehewa yenye mizigo yameachwa nyuma watamani kuyarudia, nahapo watagundua mafuta kwenye vichwa yameisha, itabidi kila mmoja arudi kwa mguu kwanjia tatu. mimi nashidwa kuelewa hawa viogozi wanafanya maamuzi hayo yote bila kuhusha wananchi wao kama vile wanaongoza wanyama. swali hii jumuiya ni kwa manufaa ya maraisi au ya wananchi? it is shame that African leaders still think

    ReplyDelete
  10. Hawa jamaa hawaitaki tz sababu wanasema mnaringia ardhi kubwa mlionayo sababu jk alikataa kulijumuisha swala ardhi kwenye jumuia ya EA, kagame hataki kuonaJk anaendelea kuisaidia serikali ya congo kuiondoa M-23 sababu ana maslai yake, lately tz imekuwa close na nchi kubwa na wamaaidi kuwekeza bongo.Tz inabidi kukomaa na uchumi wetu tujaribu kuimarisha uhusiano wa nchi kama congo, burundu na nch nyingine za kusini, hawa jamaa hwatupendi na mshangaa kibabu m7 yeye anaburuzwa tu.

    ReplyDelete
  11. Watu wengi hawafahamu siri ilyopo Rwanda na Uganda. kwa taarifa zenu huku kutengwa kwa Tanzania ni kutokana na kupeleka majeshi Congo. Kagame na Museven ndio wezi wakubwa wa rasilimali za wacongo.waasi wakidhibitiwa uchumi wa Rwanda utadidimia sana na watakuwa wasumbufu sana East Africa. La muhimu ni Tanzania kujitoa kwa sasa maana hakuna manufaa

    ReplyDelete
  12. demu kama hataki mwache aende zake usimbake niahayo tu nadhani nimeeleweka.najivunia kuwa mtanzania

    ReplyDelete
  13. Hawana lolote hao m23 wameshabanwa na hawana njia mbadala ya kupata mali so wanajidai wanaitenga tz kulipza kikas na wanajidai wanamipango ming ya maendeleo na vkao miaka yote mlikua wp au mlingoja tz ipeleke jesh congo?? Unafk 2 hatuteterek wala ham2tish na vikao vyenu. Wanafk wakubwa

    ReplyDelete
  14. hili swala sio la kuliangalia kisenge senge inahitaji busara zaidi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad