ANNA MAKINDA"WABUNGE WASTAAFU WANA HALI NGUMU-HUJA OFISINI KUOMBA OMBA

Akiongea na Spika wa Bunge la Uswisi, Maya Graf, Spika Anne Makinda amenukuliwa akisema kuwa Wabunge wengi Wastaafu wana hali ngumu kiuchumi pindi wanapomaliza muda wao.
Yumkini Wabunge wetu wastaafu huwa na hali ngumu kiuchumi baada ya kustaafu, lakini, tafsiri zaweza kuwa nyingi. Si kwamba Waheshimiwa hao hawakuwa wabunifu walipokuwa Mjengoni. Yawezekana baadhi yao wanahangaika sasa kwa vile walikuwa waadilifu sana. Hawakuiba senti za Wananchi.
Kwa kuwasengenya hata waliokuwa waadilifu yaweza walio Mjengoni sasa na wanaojitahidi kuwa waadilifu nao kuanza kukata tamaa. kwamba, hakutakuwa na tuzo ya wao kuwa waadilifu, bali masimango.(P.T)
Kwamba wameitumikia nchi bila kufanya ujanjaujanja na hivyo mitaani kuonekana wako hoi. Maana, kwa mshahara wa kawaida wa Mbunge, kwa kweli kuwa na magari na nyumba za kifahari ni jambo gumu.
Tukumbuke Wabunge hao wana familia zao za watoto wa kuwasomesha , wana pia ndugu na jamaa wanaowategemea. Achilia mbali wananchi wa majimbo yao wenye kuwataka misaada kila kukicha.
Hapa Mbunge mwadilifu kwa kiwango kikubwa hawezi kumaliza kipindi chake akiwa tajiri.
Haya, kwa masengenyo haya, Spika Makinda hatawaona tena Wabunge wenzake Wastaafu wakifika kwa wingi ofisini kwake. Maana, hata wale waliokuwa wakitaka kupita tu kumsabahi Spika, na hata kumpa ushauri wa hapa na pale, nao huenda wataogopa kuonekana ni 'omba omba'.
Na kwa Wabunge hao wastaafu nitawakumbusha wimbo wa kwenye Lizombe, ngoma ya Wangoni, na wanaweza kuingiza maneno yao wakipenda, usikike hivi; ...
" Tulipokuwa Mjengoni wee, Spika hakutusemaa..
Tumeondoka kidogooo, nyuma anatusengenyaa... Weee!"
Naam, dhiki haina mwenyewe!
Maggid.

Dar es Salaam.



Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wote wezi walishazoea starehe cc mkwanja umeisha wanahahs

    ReplyDelete
  2. Kwaiyo unamuelezea ili akupe msaada au afanyeje wenyewe walichezea hela na starehe basi wacha sasa hivi waone cha moto siwaonei huruma wanasiasa hata kidogo...Tunda la msimu

    ReplyDelete
  3. Kwa hali ilivyo sasa hv siasa za Tanzania zina nguvu kuliko sheria.kuna haja ya kuwa na chombo kinachojitegemea kama ilivyo EWURA, kwa ajili tu ya kuzibiti matumizi ya serikali. imagine mishahara ya wabunge ilivyomikubwa na hawalipi kodi Rais na mawaziri hvyo hvyo.

    ReplyDelete
  4. Huyu mama ana akili kweli..? Sasa wabunge utafananisha na walimu na madaktari baada ya kustaafu..? Watu ambao ni muhimu zaidi yao..?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Atleast hao wabunge walipataga hata na chance ya kutanuaga mjengoni, mijigari na mijitotoz................mwalimu, mkulima, doctor cjui ndo wanakua na hali gani wakistaafu kiuadilifu.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad