*Adai wadau walipaswa kupewa muda zaidi, aonya rushwa
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amemuonya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa mara nyingine tena kuacha tabia ya kufanya uamuzi wa jambo lolote bila kushirikisha pande zinazohusika.
Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mgomo wa wasafirishaji wa mizigo na abiria ulioanza Oktoba 5, mwaka huu, Pinda alisema Serikali imeamua kurejesha kwa muda wa mwezi mmoja asilimia tano ya uzito wa mizigo uliozidi kwenye mizani.
Alisema hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja.
Alisema mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao.
“Chimbuko la mgogoro huu, ni tangazo la Dk. Magufuli alilotoa Oktoba mosi, mwaka huu la kuondoa ofa ya asilimia ya uzito uliozidi, baada ya uamuzi huo wadau wa usafirishaji wa malori na mabasi waliingia kwenye mgomo na kulalamikia hatua hiyo.
“Kutokana na mgogoro huu, nililazimika kukutana na Dk. Magufuli, baadhi ya mawaziri wa wizara zenye uhusiano na masuala haya, wanasheria na wataalamu wa masuala ya usafiri na uchumi.
“Kilichoongeza mgogoro ni tafsiri ya vifungu vya sheria na kwenye kanuni ya 7 (2) na 7(3) ambacho kinaeleza wasafirishaji wa magari yenye uzito uliozidi, lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria, wanatakiwa kupunguza mzigo, kupinga na iwapo watashindwa kutekeleza, watatakiwa kulipia mara nne ya tozo za kawaida.
“Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na halikuwa sheria kamili, ndio maana limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya.
“Nakubaliana na Dk. Magufuli, wapo baadhi ya wasafirishaji ni wakorofi na hawataki kufuata sheria…ndio maana walifanya mazoea ingawa wapo wengine wazuri na hao nawapongeza sana kutii sheria.
-Mtanzania
Udaku Specially Blog
MAGUFULI NI MCHAPA KAZI KWELI HATUKATAI,LAKINI NI MTENDAJI AMBAYE MAAMUZI YAKE NI YA KUKURUPUKA MNO,YAANI AKILALA AKIAMKA ANATOA JAMBO JIPYA,SASA HAYA KAZI KWAKE,WENYE MALORI WAMEISHASEMA WANAMPELEKA MAHAKAMANI NA WAZIRI MKUU NAE AMEISHAMNAWA!
ReplyDelete''kama hamuwezi kulipa 300/= kwenye kivuko basi jaribuni kuogelea kwenda kigamboni'' ni huyu huyu maghufuli...
ReplyDeleteMBONA HIYO COMMENT YAKO HAIENDANI KABISA NA TOPIC YA LEO,KAMA NDO UNAAMKA MUDA HUU JARIBU KUISOMA TENA HIYO HABARI!
ReplyDeleteHUYO AMEKUMBUKA KAULI YA MH. MAGUFULI ALIYOITOA KWA WANANCHI WA KIGAMBONI KUHUSU KUPANDA KWA NAULI YA KIVUKO. ALIWAAMBIA WANANCHI ASIYEWEZA KULIPA 300 AOGELEE!
DeleteAcha kukosoa wenzako! Mshamba we
ReplyDeletewala makufuli hakurupuki bali anakereka na uvunjaji wa sheria kwani sheria zinawekwa lakini watumiaji wanazivunja wakiona hatua haichukuliwi wanafanya mazoea wakati niwavunjaji wa sheria mimi binafsi naona makufuli hajafanya kosa yeye amefuata sheria baada yakuona uharaibifu wa barabara unaendelea ikabidi arudi kwenye sheria wewe unaambiwa hapa hakuna njia lakini kila siku unapita siku njia ikifungwa utasema aliyefunga njia amekurupuka hebu tufuate sheria kama watu watagombana.pia barabara zikiharibika wakulaumiwa ni makufuli mtasema amejenga barabara zisizo na kiwango hamtakumbuka kuwa milori ya tani nyingi kupitakiasi ilipita hapo makufuli unafanya kazi nzuri tunakukubali
ReplyDelete