In Summary
Kauli ya shabiki huyo inakuwa mzigo kwa wachezaji wa Yanga kama, Athuman Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani, Mrundi Didier Kavumbagu na Wanyarwanda Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ kuhakikisha wanafanya vizuri na kuokoa maisha ya kijana huyo mwenye miaka 31.
SHABIKI maarufu wa Yanga, Steven Mwamwala amedai kuwa, kama wakifungwa na Simba mechi ya Jumapili ijayo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, atajinyonga.
Na akamsisitizia mcheza filamu, Wema Sepetu afike uwanjani kuona mechi ya Simba na Yanga Jumapili ili ampe zawadi yake ya jezi ya Yanga aliyoigharamia Sh45,000.
Mwamwala ana historia na Yanga ilipopigwa mabao 5-0 aliangua kilio cha nguvu na video zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli ya shabiki huyo inakuwa mzigo kwa wachezaji wa Yanga kama, Athuman Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani, Mrundi Didier Kavumbagu na Wanyarwanda Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ kuhakikisha wanafanya vizuri na kuokoa maisha ya kijana huyo mwenye miaka 31.
Aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Nimeandaa kamba ya katani kabisa, nimeificha na siwezi kusema nilipoiweka kama Yanga itafungwa mchezo huo, nitajinyonga ili kupoteza uhai wangu. Unajua inauma sana mnapofungwa, nataka timu yangu ishinde Jumapili ili niwe na amani kwa ushindi wowote ule ilimradi tutoke na pointi tatu.”
Kuhusu, Wema shabiki huyo alisema anampenda sana kama dada yake na anatamani akutane naye.
“Nimemtafuta sana na naomba siku hiyo aje kwa sababu nimemwandalia zawadi. “Nimemnunulia jezi ya Yanga na tayari nimeiandika jina la Wema, imenigharimu Sh 45,000,” alifafanua Mwamwala ambaye anaishi Tabata Segerea jijini Dar es Salaam
Mwanaspoti
Udaku Specially Blog
Wema ipo china baba
ReplyDeletewe komaa na kina mwajuma tu
Usipo jinyoga wanasimba tutakugonga na gari si umetamani kufa ww ni 3 bila ili ufe vizuri
ReplyDeletehuyu ana wazimu
ReplyDeleteNi hii mijibangi mnayovuta utotoni ndio inakusumbua kijana.
ReplyDeleteKwa Wema umekula wa Chuya kwani itabidi usubiri mpaka hapo Diamond atakapomaliza shoo zake huko China
ReplyDeletehili limjamaa tumetoka kjji kimoja alikua anaanguka kifafa msimuone hivyo shuleni alikuA taahira haelewi
ReplyDeletekwakweli vichaa n wengi. Wema anavaa milion kwa mara 1 we unatangaza nmemgharamikia jezi yake sh 45,000? Jpange bab
ReplyDelete45,000/ndio uwezo wake mwamwala bwege wewe
DeleteHuo sasa sio kupenda yanga Bali kukuta tamaa na maisha.
Deletemichezo Ni burudani na upendo wala sio kifo
duu
ReplyDeleteHuo wake ni ushabiki wa.kishamba. inavyoelekea hajui kama kwenye mpira kuna matokeo 3 yaani kishinda, kishindwa na droo. Huyo jamaa aache ushabiki wa kishamba.
ReplyDeleteJaman mbona mmenuna?inamaana hamjui kuwa dunian kuna utani?
ReplyDeleteAkamtanie mama yake. kwenye mambo ya kifo hakuna utani
DeleteHana lolote anataka sifa tu
ReplyDeleteHana lolote anataka sifa tu
ReplyDeleteHuyu mjinga ana ana clip yake hapa ktka u turn http://www.u-turn.co.tz/index.php?option=com_zoo&view=frontpage&Itemid=53&page=5
ReplyDelete