VITUKO VYA ZITTO-AHUTUBIA WANANCHI KWA KUPITIA SIMU YA MKONONI

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), juzi aliibua kituko baada ya kuwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwa njia ya simu. Zitto alilazimika kutumia njia hiyo katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora akiwa jijini Dar es Salaam, ili kuwanusuru viongozi wa chama chake waliokuwa katika ziara mkoani hapa wasipigwe na wananchi.

Viongozi walionusurika kupigwa na wananchi ni Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa aliyekuwa ameandamana na wenyeviti wa chama hicho wa mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi, Shaaban Mambo.

Dalili za viongozi hao kuwa katika wakati mgumu, zilianza kuonekana mapema katika Kijiji cha Ibambo ambapo wananchi hao walishangazwa na hatua ya Zitto kutokuwapo katika msafara huo.

Matangazo ya awali ya mkutano wa chama hicho, yaliwatangazia wananchi uwepo wa Zitto katika mkutano huo, lakini mbunge huyo hakuonekana jambo ambalo liliwafanya wananchi kutoelewa.

Katika Kijiji cha Mwendakulima umati wa wananchi uliridhika baada ya viongozi waliokuwa katika mkutano kuwaeleza kuwa Zitto atakuwa katika mkutano wa mwisho uliofanyika katika kiwanja cha mnadani wilayani Kaliua.

Baada ya wananchi kubaini kutokuwepo kwa Zitto, walizuia gari la matangazo lisiondoke na kumtaka Mtemelwa ampigie simu ili wasikie kauli kutoka kwa Zitto vinginevyo msafara wao usingeweza kutoka salama katika viwanja hivyo.

Wakiwa kiwanjani hapo, Mtemelwa na viongozi hao walianza kuhutubia lakini kelele za wananchi zilizidi wakihoji kutokuwapo kwa Zitto, ndipo Mtemelwa alipopanda jukwaani na kumpigia Zitto simu.

Mtemelwa alimweleza Zitto hatari inayowakabili baada ya kutokuwepo kwake ambapo Zitto alieleza kuwa alikosa ndege na kuahidi kurejea katika Wilaya ya Kaliua kabla ya kufanya ziara katika Mkoa wa Kigoma.

Kutokana na hali hiyo, Mtemelwa alimpigia simu Zitto na kisha kuunganisha mazungumzo yao katika kipaza sauti cha uwanjani ambapo Zitto aliwaomba radhi wananchi hao kwa hali iliyojitokeza na kuwaahidi kuungana nao wakati mwingine.

“Naomba muendelee na moyo huo huo kwa ajili ya Chadema, niliahidi kuwa nanyi leo ila nimeshindwa kwa sababu ya kukosa usafiri wa kunifikisha huko, wasikilizeni viongozi mlionao nami nitaungana nanyi wakati mwingine, nawaomba msamaha kwa hali iliyojitokeza,” alisema Zitto.

Katika hotuba yake hiyo, Zitto aliwaeleza wananchi juu ya umuhimu wa kujua haki zao za msingi na namna CCM inavyowasahau wakulima na kuwakumbatia wawekezaji huku nchi ikiendelea kubaki katika umaskini.

Kutokana na hotuba hiyo, wananchi waliohudhuria mkutano walimuahidi Zitto kuruhusu msafara kuendelea katika maeneo mengine kwa sharti la Zitto kurudi katika eneo hilo vinginevyo watakipa mgongo chama chake.

“Tumeahirisha mkutano mara tatu kila siku tunaambiwa Zitto amepata dharura ndiyo maana leo tulitaka kuwashughulikia hawa viongozi waliokuja bila Zitto,” alisema mmoja wa watu waliohudhuria.

Awali katika Kijiji cha Mwendakulima, wananchi wa kijiji hicho walieleza namna Chama cha Msingi kinavyowadhulumu fedha za mauzo ya tumbaku na kueleza kuwa wale wanaohoji juu ya malipo yao hufukuzwa katika chama.

Tayari wanachama zaidi ya 180 wameshafukuzwa katika chama hicho kutokana na kudai fedha za mauzo ya tumbaku.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ibambo, Erasto Mazinge aliwaeleza baada ya waandishi kutaka ufafanuzi wa ofisi ya Serikali kuwa katika sehemu moja na ofisi za Chama Cha Mapinduzi.

Mazinge alisema licha ya wananchi kujenga jengo hilo lenye wastani wa vyumba nane kwa matumizi ya Serikali, CCM iliamua kuwabadilikia na kulifanya ni jengo lake.

“Historia ya hapa hili jengo ni la Serikali, wenzetu wa CCM wameamua kulipora na kufanya mali yao pasipo kujali nguvu za wananchi zilizotumika,” alisema Mazinge.

Kauli ya Mazinge inaungwa mkono na John Kapongo, Katibu wa Tawi la CCM Mwongozo, aliyesema chama chake kilitumia mbinu ya kuwalaghai wananchi kujitolea kujenga jengo hilo kwa ajili ya matumizi ya Serikali.

Alisema kwa mfumo huo wa Serikali ya kijiji na CCM, kila moja kudhani jengo hilo ni mali yake, husababisha kukosekana kwa mapato ya upangishwaji wa jengo.


“Kuna chama cha Msingi kimepangisha pale na kwa uhalisia mapato ya kodi ilibidi yaende katika Serikali ya kijiji, lakini hilo tusahau ni ndoto na hata mbunge wetu hili analifahamu na hathubutu kulisemea,” alisema Kapongo.


Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zitto anatakiwa agombee urais 2015. Chadema watake wasitake tunamhitaji kamanda toka ujiji kigoma. wakizingua gombea kama independent candidate achana na wachaga hao wamejaa kila shirika tumechoka nao.

    ReplyDelete
  2. We shoga mawazo unayowaza pengine zito hawazi hayo,usigawanye upinzani we mbwa!!!unataka agombee kwa lazima? Kuna utaratibu katika kila jambo kama anataka agombee atapewa nafasi na wenzake wanaotaka pia kisha mmoja atateuliwa kati yao dats wht we call democracy!! Sio ooh Wachaga!! We unaleta ukabila kipumbavu tu mpumbavu wewe!!!!kina mbowe wangekuwa wakabila hata uyo zitto usingemjua na kumuona chadema wao ndo walileta vijana timamu kama zitto kwa manufaa ya chama,leo unawaita wakabila?? Vp umri wake unaruhusu kugombea urais? Vp independent candidate imepitishwa kisheria? Namkubali na nampenda zito ila siamini kama atatumia njia za kipumbavu kama zako kupata urais!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad