DR SLAA"TUMEGUNDUA NJAMA ZA KUIVURUGA CHADEMA"

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amesema chama chake kimegundua njama za kutaka kukivuruga.

Kiongozi huyo anayefikiriwa na wengi kama mwanasiasa mwenye nguvu kubwa nchini amesema kuna mipango imeandaliwa ya kupandikiza watu kwa lengo la kukimaliza chama hicho wakati wa uchaguzi wa ndani.

Mwanasiasa huyo amesema kwa vile chama chake kinafanya kazi kisayansi tayari kimegundua mipango yote na akawahakikishia maelfu ya wafuasi wa CHADEMA kote nchini kwamba mipango hiyo itadhibitiwa kikamilifu.

Kuhusu suala la Usaliti wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Dr Slaa amesema kwa kuwa yeye ni ngazi ya Rufaa endapo kama atalizungumzia atakuwa hamtendei haki.


Source: RAI JUMANNE.

Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna chama hapo Chadema mafisadi kama kaka zao.

    ReplyDelete
  2. Kama hakuna chama hapo, hao waliokuongoza miaka 50 na maisha ya dhiki na sifa nyingi za amani ndo chama chako?nyie endeleeni kulala na mtakoma na hao mabeberu wa ccm.

    ReplyDelete
  3. KWI KWI KWI KWISHNEY WEZI WAKUBWA NYIE

    ReplyDelete
  4. Hakuna Kiongozi yeyote mwenye moyo na Binaadamu WAPUUZI MNAANGALIA mATUMBO YENU , CHECK HAPO ULIVYOKWIVA NA MAMBO YA MARIKANI !

    ReplyDelete
  5. wanamiliki nyumba nje ya nchi ?? za mwizi arobaini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww kumiliki nyumba nje ya nchi wala sio jambo la ajabu.Mbowe familia yao toka zamani ni wapiganaji,mali nyingi karithi

      Delete
    2. Wewe acha kutetea mashudu, nani asiyeijua familia ya kina mbowe,...Baba ua alikuwa mwizi na fisadi wa kutisha enzi za nyerere!..kama ni kurithi amerithi mali za wizi na yeye anaendelea kuwaibia CHADEMA,,
      teh teh teh teh teh!

      Delete
  6. MBOWE I LOVE YOU BABY

    ReplyDelete
  7. Hakuna chama chochote chenye huruma na wananchi wote wezi,tafuteni hela muwasomeshe watoto wenu hakuna wa kuwatetea hapo ufisadi mtupu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe kama ni msomi basi usomi wako ni wa kukariri , na hujielewi! Ila ka ni layman si kosa lako kwasababu upeo wako ni mdogo. Kwa hali hii inayoendelea ndani ya CDM bado unatetea!!, Duuuh Majanga haya!

      Delete
  8. Hakuna cha kuzugana hapa,kama umegundua njama c useme? Mbona wenzenu ccm wakikosea uovu ukijulikana hua wanakil na kuwajibishana? Nyie mnakosea afu mnasingizia hujuma kama yanga na simba? Kubalini makosa mwachie madaraka na wengine waongoze,

    ReplyDelete
  9. Ni rahisi sana kuwagundua mafisadi wanapotoa maoni kuishambulia chadema na viongozi wake.HATUDANGANYIKI NG'O!!!

    ReplyDelete
  10. Ukiona mtu anaitetea ccm,mchunguze sawasawa,atakuwa cio mzima.

    ReplyDelete
  11. Mbowe mwenyewe anaomuonekano wa kimafia sasa cjui 2tarajie nn??

    ReplyDelete
  12. Hakuna anayeivuruga CDM Bw. Slaa, ni nyie msiotaka kuambiwa ukweli, mchaakachue katiba halafu mje na ngonjera, sasa unaleta za kuleta heti kuna watakaopandikizwa, au unamsema ZITTO. Atakutoa roho

    ReplyDelete
  13. nyie mnaotetea CCM mmechanganyikiwa, ndo maana maisha yenu hoi

    ReplyDelete
  14. Hakuna anaetetea ccm hapa,ccm mafisad na chadema wameshakuwa mafisad,achen ushabiki wa yanga na simba ktk mambo ya nji,chadema ni chama tuluchokuwa tunakitegemea kuleta mabadiliko,lakn makosa yanapofanyika yakishindwa kulekebishwa mapema badae chama hakitakuwa tofaut na ccm,so achen ujinga wa kumwacho mtoto achezee petrol jikon wakt mnajua kunamoto

    ReplyDelete
  15. Hivi hawa viongozi wa CDM,wanadhani kuwa watafia madarakani? Maana nashangaa kikikaribia kipindi cha uchaguzi wao wa ndani huwa wanaweweseka utadhani wanataka kukata roho vile! ama kweli sasa nimeamini ya kuwa ulafi wa madaraka ni ulevi mbaya sana tena kuliko hata wa pombe! Na je,ni kwa nini wanahitaji sana kuendelea kuwa viongozi? Au kuna maslahi gani hapo CDM kwa mtu kuwa kiongozi? ZITTO,SLAA,MNYIKA,MBOWE watakipeleka hiki chama mahali pabaya sana kwa tamaa ya madaraka.Lakini wakae wakitambua ya kwamba,Watanzania tuna imani kubwa juu ya chama hiki lakini imani yetu itaendelea kupungua iwapo tu wataendelea kuwa na misuguano juu ya ulafi wa madaraka miongoni mwao.NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  16. Moustapha Abdula Lutavi1 November 2013 at 00:34

    Dr. Slaa - "napenda kuwahakikishia wanaChadema wote nchi kwamba hakuna toleo lolote la katiba ndani ya CHADEMA inayotoa ukomo wa madaraka ya uongozi ndani ya chama."
    Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2004 ibara ya 6.3.2 kipengele cha (c) kinasema ifuatavyo "Leaders who finish their terms in office shall be eligible for re-election provided he qualifies but NO LEADER CAN HOLD THE SAME POST AT THE SAME LEVEL OF PARTY STRUCTURE FOR MORE THAN TWO TERMS".
    Kwa mujibu wa maelezo ya mroho wa madaraka (Dr. Slaa), anasema ameshiriki kikamilifu katika kuiandaa hiyo katiba. Sasa inamaana alikuwa hajui anachokiandika au hajui kiingereza nimtafsirie!!!??????.
    Naona sasa miti ishaanza kuteleza, ndo nyani anakufa hivyo,, na mtaishia kunawa tu, kula wala wengine!.

    CCM Oyeeeee!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad