JAMAA AJIKATA UUME WAKE BAADA YA MADEMU KUMKATAA KWA KIPINDI KIREFU

Jamaa mmoja nchini China ameukata uume wake mara baada kuchukizwa na hali ya kutokuwa na demu kwa kipindi kirefu, na mara baada ya kitendo hicho jamaa alikimbizwa hispitali kwa matibabu.

Alipofikishwa hospitali madaktari walimueleza wasingeweza kumsaidia sababu kipande cha uume alioukata kiliachwa sehemu ambayo alilifanya tendo hilo, hivyo ikaamuliwa arudi nyumbani kwake akakichukue ili aweze kupata matibabu.

Yang Hu, 26, alifanikiwa kurudi tena hospitali, huku akiwa na watu kadhaa, madaktari walimueleza kwamba kipande kilichokatwa kilipoteza damu nyingi sana hivyo ingeshindikana kuweza kukiunga tena.

Marafiki wa Yang walisema kila kukicha jamaa alikuwa anatingwa sana na mawazo kutokana na ukweli kwamba toka alipohamia jijini hapo hakuwahi kupata demu.

Mbaya zaidi, walisema, jamaa alikuwa akifanya kazi kwa masaa mengi kwenye kiwanda cha nguo ndani ya Jiaxing, kwenye jimbo la Zhejiang Mashariki ya China, huku wakihisi kuwa ndiyo kitu kilichomsababisha kutokuwa na muda wakukutana na mwanamke.


Msongo kichwani ulizidi kuongezeka kwa kasi, kiasi cha kumfanya kuzidi kujisikia vibaya zaidi, mnamo tarehe 27 Oktoba mara baada ya kurudi nyumbani majira ya saa 3 usiku jamaa alikodi chumba na kuamua kuukata uume wake kutokana na kuona kwamba hakikuwa ni kitu cha maama na hakikuwa na faida naye, huku akiamini kitendo hicho kingeweza kumsaidia kuacha kufikiria juu ya maswala ya mademu

Udaku Specially Blog

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nyi watu waudaku hizi habari huwa mnasimuliwa au mnatunga muuze gazeti hivi hii habari kwa akilizenu timamu inawezekanaje uipost bila kuonyesha vigezo vya ukweli mbona hakuna chombo cha habari chochote china kinarecod ya hi habari mliipataje hebu tuambieni

    ReplyDelete
  2. Hii ya kwenu wazushi wakubwa nyie, kwa china bado habari kama hiyo haipo

    ReplyDelete
  3. Kama mtu huna habari si uende kulima tu, badala ya kuandika hadithi za kutunga ukaziita za ukweli...."Anza na HADITH HADITHI...." nasi tutasoma tu, lakini msitufanye hatuna akili....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad