WANAJESHI WALIO IBA VITU WESTGATE WAKATI WANAPAMBANA NA MAGAIDI WAFUNGWA

Nairobi, Kenya. Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefutwa kazi na kufungwa jela kwa kitendo cha kupora mali wakati wa shambulizi la kigaidi kwenye Jengo la Westgate mwezi jana.  Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la Kenya, Julius Karangi.

Karangi amesema kuwa mwanajeshi wa tatu aliyeshukiwa kwa uporaji anachunguzwa.

Awali Karangi alikanusha kuwa wanajeshi walifanya uporaji kwenye jengo hilo licha ya picha za CCT kuonyesha wanajeshi wakibeba mifuko ya plastiki kutoka kwenye moja ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya Jengo la Westgate.

Hivi karibuni wanamgambo wa Somalia, al-Shabaab walikiri kufanya shambulizi hilo na kuwateka  nyara Wakenya kadhaa waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.

Watu 67 walifariki na mamia ya wengine kujeruhiwa.

Wakati huohuo, mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa uhalifu katika idara ya polisi,Ndegwa Muhoro alisema kuwa mmoja wa magaidi waliokuwa ndani ya jengo hilo walipiga simu nchini Norway wakati walipovamia jengo hilo.

Mmoja wa washukiwa wa shambulizi hilo ametajwa kuwa Hassan Abdi Dhuhulow mzaliwa wa Somalia ambaye ana uraia wa Norway.

Jeshi limesema kuwa magaidi wote wanne waliofanya shambulizi hilo waliuawa.

Udaku Specially Blog

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wajeshi walioiba westgate walikuwa sio wawili bana video inaonesha wate walioingia ndani walichukuwa vitu na kutia kwenye mifoko meipe na kuondoka bana. hao wawili wameonewa tu bana!

    ReplyDelete
    Replies
    1. usipende kuongea usichojua.kuna mali zilizookolewa, una uhakika gani kama sio hiyo mifuko myeupe?

      Delete
  2. magaidi hao wanne waliondoka usiku huo huo wa jumamosi na haijulikani waliko; hakuna aliyekufa;

    ReplyDelete
  3. hakuna gaidi alikufa wote walifanikiwa kukimbia kama kweli wamekufa wangetuonesha miili yao sisi wananchi wa kenya ili tuamini kuwa wamekufa!

    ReplyDelete
  4. Mbona jeshi la kenya halieleweki? Kwani baada ya Mohamed Ally kuonyesha video ya wanajeshi wakitoka na mifuko myeupe kwenye kipindi cha jicho pevu , huyo cjui mkuu wa jeshi alisema c kweli. Sasa iweje wawafukuze kazi? Mmmmh makubwaa

    ReplyDelete
  5. Ubabaishaji huo

    ReplyDelete
  6. Mhh au ni hasira za kutowapata magaidi mnahamishia kwa wanajeshi? shukran za punda izo kumbe ivyo vitu mlitaka waondoke navyo magaidi au viwake moto mari kwa mari.

    ReplyDelete
  7. hongera sana serikali ya Kenya. . .saaaaaaaaafiiiii!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad