ZITTO KABWE KUSHITAKIWA KWA KUUTANGAZA MSHAHARA WA RAIS NA WAZIRI MKUU

HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
  
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.

Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.
  
Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.
  
“Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.

Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.
  
“Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.

 Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.

“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
  
“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.
  
Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.
  

Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.


Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wabongo mbona munatushangaza na sheria zenu aisee huku kenya mbona ni jambo la kawaida wananchi wanajua mishahara ya viongozi wao kuanzia diwani hadi rais mimi sioni haja ya kumshtaki zitto lakini kama ni sheria ya Tz kumshtaki basi inabidi muipige msasa sheria hiyo,kwa sababu wananchi wanapaswa kufahamu mishahara ya viongozi wao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sheria wapi,,huyu nae mwenyekiti wa wafanyakazi ni mshenzi tu, mbona kila mwaka wao wanataja kima cha chini cha mshahara,,, pia wanapotangaza ajira mpya mbona wanaweka kiwango cha mshahara wa nafasi husika. Anajipendekeza tu huyo mzee

      Delete
  2. Kwa sababu walioko madarakani wezi na hawapendi ukweli. Ina boa sana stupid ass!

    ReplyDelete
  3. MSEMA KWELI HUCHUKIWA NA WENGI

    ReplyDelete
  4. mmh,naungana na mdau hapo juu...

    ReplyDelete
  5. We kiongozi wa TUGHE unataka kuficha maovu hutufai achia ngazi

    ReplyDelete
  6. ccm wezi wakubwa hawa ndo mana hawajak 2jue mishahara yao coz itz so shame 2 majority who expoloited it

    ReplyDelete
  7. Kuna tatizo gani kujua mishahara ya viongozi wa nchi kinachofichwa ni k2 gani?zito sema yote wakufunge tuone 2po nyuma yako,wanakukatisha tamaa lakini laiti wangejua wanainchi 2mechoshwa na usiri mkubwa uliopo serikalini wasingeongea,wananchi tupo nyuma yako hatuangalii vyama tunaangalia uadilifu wako kwa wananchi,je upo kutetea maslahi ya wananchi?maana hii nchi imeshikwa na wachache ni kama ya familia fulani fulani,watanzania tuamke tuangalie rasilimali za taifa hili zinawafaidisha wavuja jasho?na si vinginevyo Zitto,Mwakyembe,Dk magufuli,Mnyika,Mbowe,na wengineo wenye uchungu na nchi hii sisi wananchi tusio na vyama 2po nyuma yenu na Mungu awasimamie tutashinda.

    ReplyDelete
  8. We tughe acha upuuzi pigania mishahara ya wafanyakazi wako.mtu anapata 30m mwenzako huyo.au hao wabunge mshahara 11m unategemea atetee mfanyakazi.wacha tjjue mishahara yao ili tijue tuna tabaka

    ReplyDelete
  9. Huyu kiongozi wa tughe anadai mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa,je mwajiri wa rais ni nani? Huyu ni kibaraka tu anayejikombakomba kwa rais ili apewe kazi ya kijiweni kama ukuu wa wilaya.

    ReplyDelete
  10. TUGGE hamna ulichongea hapa ni utumbo mtupu, unataka siri ya nini? Nchini Kenya wananchi wanajua mishahara ya viongozi wao na hakuna mgawanyiko au uvunjaji wa amani uliotokea iweje itokee Tanzania kama sio kudanganyana huko, kwa taarifa yako hatudanganyiki, ZITTO usiogope tuko bega kwa Bega na wewe kupinga UFISADI achana na huyu Tugge ni wale wale

    ReplyDelete
  11. wewe kiongoz wa tughe lazima utakuwa ni mmoja wa watu wanaoifisadi nchi yetu,sijui nikutukane?na hasira na wewe kwa kuongea huo uozo wako.Jipange Mh zitto endelea kuwaumbua hao

    ReplyDelete
  12. eti mshahara ni siri ya mwajiri na muajiririwa pumbaf alie muajiri raisi ni nani kama siyo wananchi wacheni ujinga

    ReplyDelete
  13. WABUNGE SIWANA KINGA YA KUSHITAKIWA SASA TUGHE WATAMSHITAKI WAPI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad