WATANZANIA 3 WATIWA MBARONI WAKIWA NJIANI KWENDA KUJIUNGA NA AL-SHABAAB NCHINI SOMALI

Jeshi la Ulinzi la Kenya liliwatia mbaroni Watanzania watatu ndani ya Somalia wakiwashuku kuwa walikuwa njiani kwenda kujiunga na Al-Shabaab, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 20 Oktoba).

Ali Ramadhan mwenye umri wa miaka 22, Musa Daudi miaka 19 na Shabaan Bakiri Waziri miaka 21, walitiwa mbaroni baada ya kuingia Somalia kutoka Kenya na sasa wanahojiwa katika kituo cha polisi cha Kiunga.

Polisi walisema kwamba washukiwa hao walitokea Dar es Salaam, wakasafiri hadi mpaka wa Tanzania na Kenya huko Lungalung, baadaye wakaenda kwa gari hadi Mombasa, Malindi na Lamu kabla ya kuingia Somallia.

Kwa mujibu wa polisi, watatu hao walikuwa wanaelekea Kismayu kwenda kujiunga na "vita vitakatifu, walivyodai vinaongozwa na [Al-Shabaab]".


Chanzo: SabahiOnline

Udaku Specially Blog

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivi inakuwaje mtu unakosa roho ya uzalendo..???mungu tusaidie maana tunapotaka kupeleka hii nchi ni pabaya sana

    ReplyDelete
  2. Tendeni haki kwa watu wote. Acheni wizi, rushwa na unyonyaji. Ajira ziwepo kwa vijana.

    ReplyDelete
  3. HILO JESHI LA POLISI LA KENYA NI LA KISENGE SANA,KWANI LINA UHAKIKA GANI AU LIMEWAKAMATA HAO NDUGU ZETU KWA USHAHIDI GANI KUWA WANAENDA KUJIUNGA NA AL SHABAB? LENYEWE LINAACHA KUWAELEZA WAKENYA KUWA LILISHINDWA KUWAKAMATA MAGAIDI WA WESTGATE LINAANZA KUDEAL NA NDUGU ZETU.TENA WATUKOME KABISA! AMA KWELI MFA MAJI,HAACHI KUTAPATAPA!

    ReplyDelete
  4. Ww hivi mpunbavu sana kama hawaendi kujiunga basi wameenda kufanya nn huko somalia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio Kula kijana anaekwenda Somali Ni al shababy, wapo wanaokwenda kutafuta kazi.
      engine Sana ndugu zao hivyo kwenda kusalimia pia, Somali zipo kazi sehemu kibao

      Delete
  5. WEWE NI MWENDAWAZIMU KWELI,KWA HIYO WANAOKWENDA SOMALIA WOTE WANAENDA KUJIUNGA NA MAGAIDI? MBONA KIKWETE HUWA ANAKWENDA HUKO?

    ReplyDelete
  6. wewe unaesema wanaenda kujiunga na al shabab akili zako ziko makalioni, ina maana watu wasisafiri au wasitalii au unalako moyoni. Kenya na ninyi mkome kuonea watu wasio na hatia kwa sababu tofauti na mnazoziainisha kumbe mna chuki zenu na watu fulani, al shabab wenyewe mmewashindwa mnataka onea watu bule.

    ReplyDelete
  7. wewe unaesema wanaenda kujiunga na al shabab akili zako ziko makalioni, ina maana watu wasisafiri au wasitalii au unalako moyoni. Kenya na ninyi mkome kuonea watu wasio na hatia kwa sababu tofauti na mnazoziainisha kumbe mna chuki zenu na watu fulani, al shabab wenyewe mmewashindwa mnataka onea watu bule.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad