MRISHO NGASSA AHADIWA MAMILIONI ENDAPO ATAFUNGA GOLI KWENYE MECHI DHIDI YA SIMBA

WAKATI homa ya pambano la watani wa jadi ikizidi kupanda, Championi limebaini siri nzito kwenye kambi ya Yanga, kwamba mshambuliaji wa timu hiyo, Mrisho Ngassa (pichani) ataondoka na mamilioni kama akifanikiwa kufunga bao katika mchezo huo.
Akiwa kambini kisiwani Pemba, Zanzibar, ambako Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ngassa ameambiwa na tajiri mmoja mdau wa Jangwani kuwa, atapewa Sh milioni moja akitupia bao siku hiyo na kama akiongeza itakuwa mara mbili.
Tayari Ngassa ana ofa ya makamu mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Davies Mosha, ambaye amekuwa akimpa shilingi milioni moja kwa kila bao analofunga na shilingi laki tano kwa pasi ya bao.
Jana, mshambuliaji huyo alikutana na bahati nyingine, baada ya mfanyabiashara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Moses Katabalo, kumwambia kuwa kama akifanikiwa kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Simba, atampa milioni moja na akitoa pasi ya bao atapata laki tano.
Hii inamaana kuwa, kama Ngassa atafunga bao kwenye mchezo huo basi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili, moja kutoka kwa Mosha na moja kutoka kwa Katabalo, lakini akitoa pasi ya bao atajipatia milioni moja. Fedha hizo zinaweza kuongezeka kutokana na idadi ya mabao atakayofunga.
“Nimeongezewa ofa nyingine, lakini hii inahusu mchezo wa Simba na Yanga tu, Katabalo kaniambia nikifunga bao atanipa milioni moja, nikitoa pasi ya bao atanipa laki tano.

“Mechi itakuwa ngumu, lakini nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuonyesha kiwango cha juu,” alisema Ngassa ambaye ana mabao mawili kwenye ligi na pasi moja ya bao.


Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad