MWIGAMBA AANZA KUIANIKA CHADEMA..AWAONYA WANAO MWITA MSALITI

*Awaonya wanaomwita msaliti
*Dk. Slaa aibua mapya
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliyesimamishwa uongozi asema atakichafua chama hicho kama ataendelea kuitwa msaliti.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Mwigamba kukiri hadharani kusambaza waraka unaowatuhumu viongozi wa chama hicho katika mtandao wa Jamii Forum (JF), akitumia jina la Maskini Mkulima. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mwigamba aliwaonya viongozi wa Chadema wanaomwita msaliti. Alisema kama wanataka awe msaliti, yupo tayari kumwaga mambo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata kidogo. 

Mwigamba, aliyejiunga na Chadema mwaka 2004, akiwa mwanachama wa kawaida, alisema akiwa makao makuu mjini Dar es Salaam kama mhasibu mkuu wa chama, ndipo alipoanza kutambua udhaifu mkubwa wa kiuongozi ndani ya chama chake.

“Niliondoka pale makao makuu kwa mizengwe, kiongozi mmoja mkubwa kabisa alinifukuza kazi kwa kunipigia simu, tena baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Fedha,Anthony Komu akiwa nje ya Dar es Salaam na kumwagiza anifukuze,” alisema Mwigamba.

Alisema kwa bahati mbaya, udhaifu huo umeshindwa kushughulikiwa na vikao rasmi vya chama, kwani yeyote anayejaribu kukosoa ama kuhoji iwe ndani ya vikao rasmi ama nje, hutangazwa kuwa ni msaliti.

Alisema kutokana na hali hiyo, ni wajumbe wachache ndani ya Chadema, hasa kwenye Kamati Kuu, ambao wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi.

Aliwataja wajumbe hao, kuwa ni Dk. Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela na marehemu Magadula Sherembi kabla hajafariki dunia.

Hata baada ya kuondolewa Aprili, mwaka jana, alirejea Arusha na hakuwahi kujitokeza kwenye vyombo vya habari ama mitandao kuzungumzia tatizo la viongozi na uongozi ndani ya chama.

“Matatizo yaliyomo ndani ya chama ambayo wanachama wa kawaida wanaokiamini chama na viongozi wake wangeyasikia, hakika wangeweza kukata tamaa.


“Nimefanya hivyo kwa mapenzi na kwa maslahi ya chama changu, sasa kama viongozi wenzangu wanataka niwe msaliti basi waniambie hata leo nimwage ambayo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata kidogo.

-Mtanzania

Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ULIVOKUWA NA MABWANA ZAKO UNAKULA BATA ULIKAA KIMYA SASA UMEPIGWA CHINI UNATOWA SILI ZA CHUMBANI ACHA MAMBO YAKO WEWE ULIKUWA UZIJUWI SIYASA ZA BONGO WAKATI MWENZIYO ROSTAM ANA YASEMA KUHUSU SIYASA ZA BONGO UIKUWA WAPI AIBU YAKO HIYOOOOO

    ReplyDelete
  2. WEWE NI ZAIDI YA MSALITI HUNA LOLOTE HATA UKISEMA TUTAKUONA MZUSHI KWANI SIKUZOTE WAKATI ULIPOKUA NDANI YA CHAMA KWANINI HUKUYASEMA LEO UMEBURUNDA UNATAKA KUTUDANGANYA WEWE KAMA ULITUMWA UTAJIJU TUMESHA KUSHITUKIA MBONA MKO WENGI MSITUONE MAMBULULA SIKU HIZI TUMEFUNGUKA WASALITI TUNAWAJUA MSITUYUMBISHE KAMA UMESHINDANA NA WEZIO KAA PEMBENI HATUTAKI UMBEA

    ReplyDelete
  3. USHAHIDI WAKUTENGENEZA HATUUTAKI KWANINI WAKATI UKO NDANI YA CHAMA HUKUYAFIKISHA MBELE LEO UMETOKA UMATAKA KUTUVURUGA YOTE HAYO TUNAJUA UMETUMWA TUNAKUAMBIA HATA UKIYAWEKA HADHARANI HATUTAKUELEWA HUO NI UDAKU TUMESIKIA HABAARI ZA UFISADI WA VYAMA VINGINE LAKINI MBONA BADO VINAENDELEA KAMA KAWAIDA ITAKUWA WEWE TU MESHA WAZOEA KWA KUHARIBIA WEZENU

    ReplyDelete
  4. Hizo comment tatu za mwanzo zote zimeandikwa na mtu mmoja tena hyo alomfukuza kazi, hyo kiongoz wa chadema... Acha kuwaandikia wananchi comment ww mshamba!!

    ReplyDelete
  5. kweli hata mwandikowao unafanana

    ReplyDelete
  6. Mwaga data zao wala usiogope mtu, hakuna mtu ambaye yuko above the low hapa tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. we mwigamba hama chadema wababaishaji njoo huku cuf hakuna majungu

      Delete
  7. huyo aliyeandika comment 3 za juu ni mwehu! anawaza kwa kutumia makalio nahic! usaliti kuongea ukweli?! mdogo wako hawez kukwambia live shemeji anakusaliti kama aliwahi kukuona ukigombana na mama kisa uliambiwa kitu kuhusu mkeo, mwenye akili atakuwekea barua mlangoni ukisoma ujumbe umefika! sasa ukijua mwandiko wake ukamuuliza akikili sio msaliti si alitaka ujue!? angekua msaliti angepinga ukitaka ushahid anao sa unataka nini!?,
    viongoz cdm kweli wa wamechakachua katiba haina ukomo wa uongoz kwa maslai yao wakati kipengele hakikuondilewa wakati wa marekebisho, nyi mmeng'ang'ana msaliti baada ya kutake point mchukue hatua!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad