WADAU WABARIKI NDOA YA WEMA SEPETU, DIAMOND
14
October 18, 2013
Na Shakoor Jongo
Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.
Mwingine aliandika: “Nadhani Penny angejiweka tu pembeni awaache hawa wawili, ni mastaa kwa fani zao, yeye angeendelea tu na kazi yake ya utangazaji. Kwanza kwake ni maumivu tu kuwa na msanii ambaye ana shughuli nyingi za kisanii, bora wale wenyewe wanajuana.”
Ingawa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa, ‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha kurudiana mara kwa mara.
-GPL
Udaku Specially Blog
Tags
acha waoane waondoe nuksi ya kufuatwa fuatwa. Panny ajute tu hana chake, kwanza hana hata pozi mshamba yule
ReplyDeleteWape wape wapeeeee!!! Peny ndo nani kwnza,kwisha habari yke kwnza hamkamilishi Diamond,Wewma ndo mpango mzima kwa kaka Diamond...
ReplyDeleteWanameelemeta..wanaamelemeta kaka Diamond na dadaa Wema...wanamelemeta..na team Wema wanamelemeta sema wanameelemetaaaaa!!!!!
ReplyDeleteKwanza peny ndiyo mdudu gani, mbona me simtambua? Alikua anaonja moto kwa ulimi, acha umuunguze. Wema na dimond mpango mzima. Peny rudi tanga ukalime miogo
ReplyDeleteWanameremetaaaaaaa wapi kibwaya mie nicheze mdundikooo km nawaona siku hyo team,haha tutalewajeeeeeee
ReplyDeletewap timu Wema !!!!!!!!!!!!!!! kitu hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hiphip hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHahahaha namuonea huruma penny
ReplyDeletepenny ndo mpango mzima.
ReplyDeletepenny mtafute wakwako akupendae kwa dhati diamond mchafuzi ustaa unambeba utapoteza mda wako kumpenda asiyekupenda dada....
ReplyDeletePenny kizungu ni biki atafute karatasi aandike
ReplyDeletealvyoenda pltnmz kwa penny aljua kuwa yy ndo mwanamke wa ukweli,(what goes aroun comes around).
ReplyDeleteWapi wew mbona atakoma na team yake bbuuuuuuu....!!!!!!!! Ones again 4team Penny
ReplyDeletepenny!!!! mshamba
ReplyDeleteJAMANI MWACHENI DADA WA WATU...PENNY 'PENNY ' PENNY MUNGU NDIYE MPANGAJI HASA WA KUMPATIA MTU MKE MWEMA. ...!! KAMA NI WEMA KWA DIAMOND HAYA.....!!! NA KAMA NI PENNY KWA DIAMNOD HAYA...AU KAMA NI NANILIII KWA DIAMOND HAYA....!!! CHA ZAIDI TUWAOMBEE NA TUMUOMBEE ZAIDI KIJANA APATE MKE MWEMA NA ATAKAYEMPENDA KWA DHATI
ReplyDelete