"NISAIDIENI, NATESEKA" ALIA MTOTO SELEMANI

HAKIKA ni mateso, tena makubwa. Mtoto Selemani Rajabu mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Ukonga kwa Guta, jijini Dar yuko katika mateso makali baada ya mguu wake mmoja kuvimba mithili ya tairi la gari kiasi kwamba hawezi kufanya jambo lolote zaidi ya kujiburuza tu.
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwao akiwa na simanzi kubwa, kijana huyo amesema kwamba anakumbuka amezaliwa akiwa na ulemavu kidogo chini ya nyayo za miguu yake ambazo zilikuwa nene kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea na badala yake akawa ni mtu wa kutambaa tu.
Alisema wakati huo alikuwa akiishi na wazazi wake wote wawili, lakini baadaye wazazi hao walitengana na kumfanya aishi na mama yake huko Pugu Kajiungeni. Kutokana na uwezo duni wa mama yake, alimpeleka hospitali mara moja tu, licha ya mguu wake kuendelea kuvimba kila siku.


“Nakumbuka mama yangu aliwahi kunipeleka hospitali mara moja tu nilipokuwa mdogo, lakini sikumbuki kama aliwahi kunipeleka tena,” alisema Selemani akiwa na sura ya kukata tamaa.
Alisema tangu wakati huo, mguu wake uliendelea kuvimba siku hadi siku mpaka akashindwa hata kutambaa kama mwanzo na sasa akalazimika kujiburuza licha ya uzito mkubwa wa mguu wake kutokana na kuongezeka kwa uvimbe.
Kutokana na hali hiyo kuzidi kuwa mbaya, alisema mwaka jana mama yake alimpeleka Hospitali ya CCBRT ambako baada ya madaktari kumuangalia walisema mguu wake hauna maji ambayo wangeweza kuyanyonya ili kuyatumia kupata vipimo na kujua tatizo linalomsumbua.
Hata hivyo, kwa bahati mbaya, mama yake mzazi alifariki na kumlazimu baba yake kwenda kumchukua na kumpeleka kwa bibi yake huko Manzese.


Hali ya bibi haikuwa nzuri kiafya, hivyo baba alinichukua tena na kuishi naye kwake nikiwa na mama wa kambo,” alisema Selemani. 
Mtoto huyo analalamika kuwa anatamani hata mguu wake huo ukatwe kutokana na adha anayoipata kwani anakosa raha kama watoto wengine wanaotoka nje wenyewe tofauti na yeye anayetolewa kwa kuburuzwa na watu zaidi ya wawili.
“Siku zote na raha kunapokucha najiona kama sina thamani, natamani hata mguu huu ukatwe, siwezi kufanya kitu chochote, natamani kuwa kama watoto wenzangu,” alisema.
Licha ya adha hiyo, Selemani alisema kingine kinachomuumiza ni kufanya haja zote  sehemu alipokaa na hivyo kutoa wito kwa wasamaria, akiwemo Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili aweze kupata matibabu.
Kwa wenye nia ya kumsaidia mtoto Selamani, kwa matibabu au chakula, wanaombwa kuwasiliana na chumba cha habari kwa simu namba 0713 612 533. 

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kikwete uko wapi we c ulimsaidia ray c alipokua teja? Angalia mtoto huyu

    ReplyDelete
  2. HAWA NDIO WANAOHITAJI MSAADA HASWAA KWANI MATATIZO YAO HAYAJALETWA NA MIKONO YAO WENYEWE.
    POLE KIJANA.

    ReplyDelete
  3. HIVI NYIE MATJIRI WA DAR HAMUONI KAMA KIJANA ANATESEKA NA KIKWETE PIA ULIMSAIDIA RAY C MBONA UNASHINDWA KUMAIDIA HUYU KIJANA

    ReplyDelete
  4. Pole mdogo wangu M''Mungu akusaidie upate nafuu namwisho upone.

    ReplyDelete
  5. Pole mdogo wng mungu atakusaidia utapona 2. Kikwete c ray 2 isitoshe huyu kazawaliwa na tatzo kulko huyo teja aliyejitakia.

    ReplyDelete
  6. pole sana mdogo wetu kila kitu hupangwa na MUNGU.

    ReplyDelete
  7. Eeeh Mungu Baba kiponyeshe kiumbe chako..hakika anateseka

    ReplyDelete
  8. Hakika nitatoa hata kama ni shilingi moja,,kwasababu hii ni hali mbaya kwa mdogo wangu huyu,,nina uhakika wote sisi bila kusema kikwete au matajiri,hata sisi wenye uwezo wa kutembea na kukusanya japo buku moja yaani 1000 tunaweza kwa pamoja,,kama tunaweza kuweka hela kwenye simu zetu na kusoma haya magazeti online au hata ukalipa 2000 ukaingia kwenye internet basi hatushindwi kufanya jambo,, naomba tukitaka kusaidia tusiangalie wenye uwezo, mi nadhani hata kidogo kinafaaa kwani kidogo kidogo hujaza kibaba..pls ! Tuma chochote..najihisi kama huyu ni ndugu yangu/yako wa kuzaliwa utajiskiaje?au utafuraje utakapoona hata mtu katoa 2000 kwa roho safi..pls lets do something for this poor boy...#Mako

    ReplyDelete
  9. Daaa inauma sana,

    ReplyDelete
  10. Dah! Pole sana kaka Mungu yupo pamoja nawe utapona tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad